Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Mhispaniola akoshwa na vipaji vya Kitanzania

KOCHA Pict

Muktasari:

  • Katika mazungumzo yake na Mwanaspoti, Linares alieleza kushangazwa kwake na kile alichokiona kwa Sylvanus Marwa na Iddy Mataka makinda wawili wanaowakilisha Tanzania kwenye kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 16.

KOCHA wa akademi ya The Spain Rush-SPF, Mhispaniola Vicente Linares, ameongea jambo baada ya kushuhudia uwezo wa vijana wawili wa Kitanzania waliopo katika akademi hiyo mjini Valencia, Hispania.

Katika mazungumzo yake na Mwanaspoti, Linares alieleza kushangazwa kwake na kile alichokiona kwa Sylvanus Marwa na Iddy Mataka makinda wawili wanaowakilisha Tanzania kwenye kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 16.

“Hawa watoto wana kitu tofauti,”  alisema Linares kwa msisitizo.

“Marwa ni mshambuliaji mwenye nguvu, akili ya kucheza, na anajua wakati gani abadili kasi ya mchezo. Mataka naye ana uhodari mkubwa anaweza kucheza kama winga au namba tisa. Kitu kikubwa ni kwamba wana kiu ya mafanikio.”

Marwa alizaliwa Septemba 29, 2008 na anacheza kama mshambuliaji wa kati, huku Mataka, aliyezaliwa Mei 17, 2015, akionyesha uwezo wake katika nafasi ya mshambuliaji na pia winga.

Linares, amesema uwezo wa vijana hao umemfungua macho kuhusu hazina iliyopo Tanzania. “Kama hawa wawili ni mfano wa vipaji vilivyopo Tanzania, basi kuna kitu kikubwa tunapaswa kukiangalia huko. Nimevutiwa sana. Nataka kuona zaidi,” alisisitiza kocha huyo.

Kutokana na hamasa hiyo, kocha huyo ameweka bayana kuwa atashiriki kikamilifu katika kambi maalum ya mafunzo ya soka itakayofanyika majira ya kiangazi kati ya Juni hadi Agosti 2025 jijini Valencia, Hispania.

Kambi hiyo imelenga vijana wenye umri kati ya miaka 12 hadi 21 kutoka sehemu mbalimbali duniani, ikiwamo Tanzania, na itakuwa na mafunzo ya soka na ya lugha ya Kihispania.

Kwa mujibu wa waandaaji wa Spain Rush-SPF, vijana watakaoshiriki watapata nafasi ya kucheza mechi za kirafiki dhidi ya akademi mbalimbali za Hispania na pia kufanya majaribio mbalimbali nchini humo.

Kwa vijana wa Kitanzania wanaotamani kufuata nyayo za Marwa na Mataka, fursa hiyo ipo wazi. Maombi ya kushiriki yanatumwa kupitia tovuti rasmi ya akademi hiyo, spanishprofootball.