Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kilichomponza Kijuso hiki hapa

Kijuso Pict

Muktasari:

  • Kijuso alifikia uamuzi huo ikiwa ni baada ya timu hiyo kuchapwa mabao 3-0 na ‘Chama la Wana’ Stand United Desemba 20, mwaka huu kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga hivyo, kujiweka pembeni na kikosi hicho.

ALIYEKUWA kocha wa Cosmopolitan, Mohamed Kijuso amesema sababu za kufikia makubaliano ya pande mbili ya kuachana na timu hiyo ni kutokana na mwenendo mbaya, ingawa hajashindwa kutengeneza kikosi bora kinachoweza kuleta ushindani msimu huu.

Kijuso alifikia uamuzi huo ikiwa ni baada ya timu hiyo kuchapwa mabao 3-0 na ‘Chama la Wana’ Stand United Desemba 20, mwaka huu kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga hivyo, kujiweka pembeni na kikosi hicho.

“Ni makubaliano ya pande mbili kwa sababu hakuna jinsi zaidi ya hapo tulipofikia, nawashukuru viongozi kwa nafasi hiyo waliyonipa na nawaombea wafanye vizuri katika michezo iliyobaki, naamini wana wachezaji wenye uchu wa mafanikio.”

Kijuso msimu huu hadi anaondoka ndani ya kikosi hicho amekiongoza katika michezo 13 ya Ligi ya Championship, ambapo kati yake ameshinda miwili, sare miwili na kupoteza tisa, akikiacha kikiwa nafasi ya 14, kwenye msimamo na pointi nane.

Makocha wengine walioondoka kwa sababu mbalimbali ni Mussa Rashid wa Biashara United, Twaha Beimbaya (Kiluvya United), Meja Mstaafu Abdul Mingange (Stand United), Ivo Mapunda (Songea United) na Ally Ally (Transit Camp).