Kiduku aporomoka viwango vya ndondi

Thursday June 10 2021
kiduku pic
By Imani Makongoro

BONDIA Twaha 'Kiduku' Kassim ameporoka kwa nafasi nne kwenye viwango vya ndondi nchini.

Kiduku licha ya kuwa namba moja kati ya mabondia 13 kwenye uzani wa super middle, katika ubora wa mabondia wa kila uzani 'pound for pound' ya Tanzania ameporoka hadi nafasi ya nane.

Awali Kiduku alikuwa ni namba nne kwenye pound for pound ya Tanzania, nafasi ambayo sasa inashikiliwa na Salum Mtango mwenye nyota mbili na nusu.

Mwaka huu Kiduku amecheza mapambano matatu na kupigwa mara mbili kwenye pambano la Mei 20 dhidi ya Bek Nurmaganbet na lile la Februari 26 dhidi ya Ulugbek Sobirov nchini Misri na Russia, alimchapa Bebe Rico Tshibangu Aprili 9 jiji Dar es Salaam

Mtandao wa dunia wa ngumi za kulipwa (Boxrec) umemtaja Hassan Mwakinyo bondia wa uzani wa super welter kuwa namba moja akifuatiwa na Ibrahim 'Class' Mgender anayepigania uzani wa super feather na Tony Rashid bondia wa uzani wa super bantam anahitimisha tatu bora ya Tanzania.

Fadhili Majiha anayepigania uzani wa super bantam amekamata nafasi ya tano, akifuatiwa na Muksini Swalehe (Mastik the don) anayepigania uzani wa feather, Innocent Evarist, Kiduku, Abdallah Pazzy 'Dullah Mbabe' na Hamisi Maya amehitimisha 10 bora.

Advertisement

Mbabe ambaye mwezi ujao atazichapa na Kiduku pia ameporoka kwa nafasi nne kutoka ya tano aliyokuwepo awali na sasa ni bondia namba tisa kwenye pound for pound nchini.

Advertisement