Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KATISHA : Kwa Tambwe mastraika watasubiri sana

Muktasari:

Kitenge alifunga hat-trick hiyo licha ya timu yake Stand United kupokea kipigo cha mabao 4-3 kutoka kwa Yanga katika mchezo wa Septemba 16 Uwanja wa Taifa jijini Dar.

WAKATI Mrundi, Alex Kitenge akiweka rekodi ya kufunga hat trick ya kwanza msimu huu,tayari wachezaji wa kigeni wameonekana kuwafunika wazawa.

Kitenge alifunga hat-trick hiyo licha ya timu yake Stand United kupokea kipigo cha mabao 4-3 kutoka kwa Yanga katika mchezo wa Septemba 16 Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Ikiwa ni miaka mitano imepita tangu mwaka 2013, wageni wamepiga hat trick 12 huku wazawa wakifunga tisa.

Amiss Tambwe ameendelea kushikilia rekodi bora ya kufunga hat trick akiwa amepachika wavuni mabao 21 kwa njia hiyo.

Tambwe raia wa Burundi amefunga hat trick sita akifuatiwa na Obrey Chirwa na Emannuel Okwi waliofunga mbili kila mmoja.

Wageni wengine waliofunga hat trick ni Mganda, Hamis Kiiza aliyefunga moja sawa na Kitenge.

Tambwe

Tambwe ambaye hivi sasa amekuwa akisugua benchi kutokana na kuteswa na majeraha ya muda mrefu alianza kufunga hat trick yake ya kwanza Septemba 18 2013 wakati huo akiichezea Simba na kuibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Mgambo JKT huku yeye akipachika wavuni mabao manne.

Pia, alifunga tena Februari Mosi 2014 alipofunga mabao matatu akiiongoza Simba kuichapa Oljoro JKT mabao 4-0.

Mshambuliaji huyo akatimkia Yanga ambapo pia aliendeleza rekodi yake ya kuzifumania nyavu na Aprili 8,2015 alifunga mabao matano alipoiongoza Yanga kuifanyia mauaji Coastal Union kwa kuitandika mabao 8-0 halafu Aprili 27 mwaka huo akafunga hat trick yake ya nne katika ushindi wa Yanga wa mabao 4-0 dhidi ya Polisi Morogoro.

Alifunga tena hat trick Desemba 19,2015 wakati Yanga ilipoichapa Stand United mabao 4-0 kisha akafunga tena mabao matatu akiiongoza Yanga kuichapa Majimaji mabao 5-0 Januari 21,2016.

Obrey Chirwa

Chirwa raia wa Zambia ambaye hivi sasa ametimkia uarabuni,alifunga hat trick yake ya kwanza Novemba 18,2017 akiiongoza Yanga kuichapa Mbeya City mabao 5-0 na kurudia tena kufanya hivyo Februari 6,2018 Yanga ilipoifunga Njombe Mji mabao 4-0.

Emmanuel Okwi

Mganda Okwi alianza kufunga hat trick 22 Aprili 2015, akiiongoza Simba kuitandia Mgambo JKT Mabao 4-0 kisha akafunga tena Simba ilipoichakaza Ruvu Shooting mabao 7-0.

Hamis Kiiza

Kiiza raia wa Uganda naye yumo katika rekodi ya wachezaji waliofunga hat trick kwenye Ligi Kuu Tanzania akifanya hivyo Septemba 21,2015,Simba ilipoifunga Kagera Sugar mabao 3-1.

Wazawa sasa

Mwagane Yeya

Mshambuliaji huyu wa zamani wa Mbeya City ambaye kwa sasa amejikita katika fani yake ya ualimu wa shule alifunga hat trick Novemba 7,2013 Mbeya City ikitoka sare ya mabao 3-3 na Azam FC.

Mrisho Ngasa

Ngassa amefunga hat-trick moja akiiongoza Yanga kuifunga JKT Ruvu mabao 5-1, Aprili 16,2014.

Ibrahim Ajib

Ajib amefunga hat trick mara mbili akifanya hivyo akiwa na timu yake ya zamani ya Simba. Timu hiyo ilishinda mabao 5-0 dhidi ya Prisons katika mchezo uliofanyika Februari 28,2015 na dhidi ya Majimaji iliposhinda mabao 6-1 Oktoba 31,2015.

Kelvin Sabato

Sabato Oktoba 22 mwaka 2016 alifunga hat trick katika sare ya mabao 3-3 kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Stand United.

Mbaraka Yuusph

Mchezaji huyu ambaye kwa sasa anaichezea Azam FC, alifunga hat trick Machi 13, 2016 akiiongoza Kagera Sugar kuichapa Coastal Union mabao 3-0.

Abdulrahman Mussa

Mchezaji huyu ambaye aliibuka mfungaji bora msimu wa 2016/2017 akipachika mabao 14 sawa na Simon Msuva alifunga hat trick msimu huo katika mchezo dhidi ya Majimaji,Ruvu Shooting ikishinda mabao 4-1.

Michael Aidan

Aidan alifunga hat trick Desemba 13,2015,JKT Ruvu ilipoichapa Prisons mabao 4-1.

Wazir Junior

Mchezaji huyu ambaye kwa sasa anaichezea Azam, Desemba 12,2015 alifunga hat trick akiiongoza Toto African kuifunga Majimaji mabao 5-1.