Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Guardiola aukubali unyama wa Ribery

Muktasari:

  • Ilipofika saa 8 usiku, Pep aliingia stejini na kuwafanya wengi kubaki kwenye mshangao mkubwa kwa sababu kitu ambacho walikizoea kutoka kwa kocha huyo kumwona tu akiwa ameketi na marafiki zake na kuzungumza mambo mbalimbali, hasa yanayohusu soka.

TOLEO lililopita kwenye Kitabu cha Pep Confidential, Mwandishi Marti Perarnau alielezea tukio lililoshangaza wengi kwa Kocha Pep Guardiola kujumuika kucheza akifurahia mafanikio ya timu yake, leo hii anaendelea kulichambua tukio hilo na mengineyo. Endelea…

Ilipofika saa 8 usiku, Pep aliingia stejini na kuwafanya wengi kubaki kwenye mshangao mkubwa kwa sababu kitu ambacho walikizoea kutoka kwa kocha huyo kumwona tu akiwa ameketi na marafiki zake na kuzungumza mambo mbalimbali, hasa yanayohusu soka.

Tukiwa Marakesh kwa mfano baada ya kushinda Kombe la Dunia la klabu, Pep alifurahia mafanikio hayo kukaa pamoja kwa ajili ya mazungumzo na watu wake wa karibu Salai Martin na David Trueba.

Kimsingi jioni hiyo hakuna kati yao aliyekuwa na hamu ya kucheza ni Cristina, mke wa Pep na Maria mtoto wake mkubwa pamoja na mama wa Cristina na mke wa Salai Martin. Hapo hapo Dante na Rafinha, Wabrazil wanaosifika kupenda kufurahia mafanikio waliungana nao.

Hata hivyo, kwa Berlin mambo yalichukua sura tofauti, David Alaba alijigeuza msimamizi wa muziki, akijifanya ndiye DJ na muimbaji kiongozi na kwa mara ya kwanza katika kazi yake ya ukocha, Pep aliamua kuinuka na kuanza kucheza na wachezaji wake.

Ilikuwa ni kwa jioni hiyo tu aliamua awe mmoja wao, baada ya kunywa kidogo aliamua kujiachia, katika kipindi fulani jioni hiyo, Ribery alimshika shingo na kumwambia kitu.

“Nakukubali Pep, umo ndani ya moyo wangu, mimi ni mtoto wa mtaani, lakini utaendelea kuwa ndani ya moyo wangu, katika maisha yangu sijawahi kufikiria kama ningeweza kujifunza zaidi ya nilivyojifunza mwaka huu.”

Sherehe ziliendelea, kwa Pep kujumuika wachezaji wake usiku kabla hakujapambazuka wakati baadhi ya wachezaji hao tayari walianza harakati za kufikiria mambo ya mlo wa asubuhi.

Wakiwa kwenye ndege kwa safari ya nyumbani Munich, kila mmoja alionekana kuguswa na mwenye uchovu, manahodha wa timu nao walirudia mara kwa mara kumuomba Pep afute mazoezi ya asubuhi siku iliyofuata, hatimaye kocha naye alikubali, mafanikio yao kwenye ligi yaliwapa muda wa mapumziko.

Nilikuwa na shauku ya kuiona timu katika mazoezi yake ya kwanza baada ya mapumziko, baada ya ushindi kuwateka hisia, je, watakuwa katika hali ya kuridhika na kubweteka na ushindi, je, wataona ushindi wao kama kichocheo cha kusaka mafanikio yajayo au ndio hadithi ilikuwa imefikia mwisho wake.

Kilichotokea ni kwamba wachezaji walikuwa na shauku ya hali ya juu, hususan Schweinstiger ambaye aliibuka mazoezini kichwani akiwa amevaa kitambaa chenye picha ya bingwa wa michezo ya kwenye barafu, Felix Neureuther.

Masikhara yote na mazingira ya utani yalikoma mara baada ya Pep kuwasili, alianza na mazoezi ya kupasha misuli moto, baada ya hapo Pep akawapanga wachezaji katika makundi matatu ya wachezaji saba saba ambao walicheza kwa dakika nne au tano, kwa maeneo madogo mkazo ukiwa kwenye kasi zaidi.

Haikutokea kwa mchezaji kuzembea au kufanya zoezi taratibu, kuna wakati Pep alinifuata na kuninong’ongeza, “Nimefurahishwa, Ribery yuko katika ubora mwaka huu, jamaa ni mnyama, ni mnyama hasa.”

Kwa hiyo nilikuwa mwenye ushahidi wa mazoezi ya kwanza baada ya mafanikio na ilikuwa wazi ilikuwa ni timu ambayo bado ina njaa ya mafanikio.

Ni timu ambayo kila mchezaji mmoja mmoja alikuwa akipambana kuwania nafasi yake katika kikosi cha kwanza, kulikuwa na ratiba ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na hakuna ambaye alitaka kuachwa benchi, katika hatua hii hakuna ambaye shughuli waliyokuwa wakijiandaa kukutana nayo mbele ya Real Madrid.

Wakati taji la ligi tayari likiwa mkononi mwao, na ligi ya mabingwa ikiwa katika harakati, niliona ni wakati mzuri wa kukaa meza moja na Pep.

“Kipindi cha hovyo msimu huu kwetu ni dakika 10 za kwenye Uwanja wa Emirates na Arsenal, Manu (Neuer) alitubana,’’ alikumbushia Pep.

“Kipindi bora cha msimu nadhani ni katika mechi dhidi ya City mjini Manchester au niseme ni dakika 40 za kwanza katika mechi na Hertha Berlin mjini Berlin.”

Itaendelea Jumamosi ijayo…