Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dili la Willy Essomba Onana Qatar latibuka

Onana Pict
Onana Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo aliyefunga mabao manne ya Ligi Kuu Bara msimu uliopita, ilielezwa angejiunga na Muaither inayoshiriki Ligi ya Qatar (Qatar Stars League) lakini inadaiwa dili hilo limekwama na sasa anajiunga na Al Ahli Benghazi ya Libya.

ALIYEKUWA mshambuliaji wa Simba, Mcameroon Willy Essomba Onana yuko katika hatua za mwisho za kukamilisha dili lake la kujiunga na Al Ahli Benghazi ya Libya, baada ya dili la kujiunga na Muaither ya Qatar kubuma.

Nyota huyo aliyefunga mabao manne ya Ligi Kuu Bara msimu uliopita, ilielezwa angejiunga na Muaither inayoshiriki Ligi ya Qatar (Qatar Stars League) lakini inadaiwa dili hilo limekwama na sasa anajiunga na Al Ahli Benghazi ya Libya.

Onana aliyefanya maandalizi ya msimu 'Pre Season' na Simba ikiwa jijini Ismailia Misri kabla ya kukatwa dakika za mwisho  ili kumpisha kipa Moussa Camara kutoka AC Horoya aliyekuja kuchukua nafasi ya Mmorocco Ayoub Lakred aliyeumia akiwa kambini katika maandalizi ya msimu mpya.

Camara alisajiliwa ili kuongeza nguvu eneo la kipa baada ya Ayoub kuumia huku viongozi wa Simba wakiwa hawana imani na makipa wengine kikosini wakiongozwa na wazawa, Hussein Abel na Ally Salim ambao wameshindwa kabisa kuonyesha ushindani.

Onana aliyejiunga na Simba Julai 5, mwaka jana akitokea Rayon Sports ya Rwanda ambayo aliibuka mfungaji bora baada ya kufunga jumla ya mabao 16 na kuasisti mengine matano, alikatwa ili kukidhi kigezo cha wachezaji 12 wa kigeni.

Nyota huyo mbali na kuibuka mfungaji bora akiwa na Rayon Sports ila alikuwa mchezaji bora wa msimu wa Ligi Kuu ya Rwanda (MVP), na kuwavutia mabosi wa Simba waliomsajili japo ameshindwa kuwashawishi na kupewa mkono wa kwaheri msimu uliopita.