Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CV ya kipa mpya wa Simba ni hii

Muktasari:

  • Kipa huyu mwenye umri wa miaka 29, jina lake ni Jefferson Luis Szerban de Oliveira Junior ana urefu wa mita 1.9 na kabla ya kujiunga na Simba alikuwa akiitumikia Rosenda FC ambayo inashiriki Ligi Daraja la nne, Brazil.

LEO Simba imemtambulisha kipa kutoka Brazil Luis Jefferson ikimsainisha mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo hadi mwaka 2025.

Kipa huyu mwenye umri wa miaka 29, jina lake ni Jefferson Luis Szerban de Oliveira Junior ana urefu wa mita 1.9 na kabla ya kujiunga na Simba alikuwa akiitumikia Resende FC ambayo inashiriki Ligi Daraja la nne, Brazil.

Hata hivyo, tangu aliposajiliwa na Resende mwaka 2017 muda mwingi alikuwa akitolewa kwa mkopo kwenda timu mbalimbali hadi kufikia hatua ya kutua Simba.

Luis ametolewa kwa mkopo kwenye jumla ya timu tano tofauti ambazo alikuwa kwa nusu msimu ama msimu mmoja pekee.
Timu hizo tano ambazo fundi huyu alipelekwa kucheza kwa mkopo ni pamoja na Athletic, Itabaiana, Volta Redonda, SC Aymores na Itabirito FC-MG.

Kwa msimu uliopita akiwa na Resende, kipa huyu amecheza mechi 21 za michuano yote akaruhusu mabao 35 na akamaliza mechi tatu bila ya nyavu zake kutikisika.