Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cristiano Ronaldo akumbuka alipolia fainali za Euro 2004

Muktasari:

Pamoja na hali hiyo bado hakukuwa na cha kumzuia kufunga bao la mwisho na la ushindi yakiwamo hayo maumivu ya goti, ni penalti iliyompa nafasi ya kutamba kwa kila namna. Masikini kipa wa Atletico, Thibaut Courtois ambaye aliruka upande wa kushoto na mpira kwenda nyavuni upande wa kulia

KATIKA toleo lililopita, mwandishi, Luca Caioli alielezea namna ambavyo Cristiano Ronaldo alishindwa kujizuia kulia mbele ya mtoto wake na familia yake wakati akikabidhiwa tuzo ya Ballon d’Or. Sasa endelea…

“Hakika yale yalikuwa machozi ya kweli,’’ baadaye alisema, “Mtoto wangu alipopanda jukwaani nilijiwa na hisia na ziliongezeka zaidi nilipoona familia yangu ikitokwa machozi, sikutaka kulia lakini mimi sikuundwa kwa jiwe.

Miezi mitano baadaye, Juni 24, 2014, Ronaldo alikutana na tukio ambalo hatokaa alisahau pale alipoinua taji la 10 la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa Real Madrid mjini Lisbon kwenye Uwanja wa Da Luz, uwanja ambao ulikuwa na maana kubwa kwa mchezaji huyo.

Ni heshima ya kipekee katika safari ya mafanikio na kupata kombe ambalo wamekuwa wakiliota kwa miaka 12, hakucheza katika kiwango chake bora kwenye mechi ya fainali dhidi ya Atletico Madrid kutokana na maumivu ya hoti la mguu wa kushoto.

Pamoja na hali hiyo bado hakukuwa na cha kumzuia kufunga bao la mwisho na la ushindi yakiwamo hayo maumivu ya goti, ni penalti iliyompa nafasi ya kutamba kwa kila namna. Masikini kipa wa Atletico, Thibaut Courtois ambaye aliruka upande wa kushoto na mpira kwenda nyavuni upande wa kulia

Ni goli ambalo halikuleta tofauti kubwa kwa sababu lilipatikana katika dakika 120 wakati tayari ubao ulishaonyesha Real Madrid kuwa mbele kwa mabao 3-1.

Hali hiyo haikumfanya Ronaldo atulie badala yake alishangilia kama vile lilikuwa bao muhimu la maisha yake, alijiweka mbele ya kamera na hivyo kuonekana na mashabiki duniani kote.

Akiwa kifua wazi mikono kiunoni, alijitanua na kuonyesha alivyo na mwili wa kiuanamichezo na kufanya kama anatoa sauti ya kuunguruma.

Ilikuwa ni kama vile alifanya jambo la ziada wakati ambao wapinzani wao walikuwa wameshagaragazwa na kujichokea, je hiyo ndiyo ilikuwa sababu ya Ronaldo kufurahia katika namna iliyopitiliza?

Ni tukio ambalo lilipangwa mapema, alilihitaji kwa ajili ya makala maalum ya Ronaldo iliyotayarishwa na kampuni ya Universal. Ni kwa nini asiitumie fursa ya biashara na mashabiki?

Ronaldo alilibeba kombe hilo ikiwa ni baada ya miaka sita tangu afanye hivyo akiwa na Man United lakini zaidi ya hilo amebeba taji katika jiji ambalo mambo yote yalianzia, ni katika uwanja ambao miaka 10 iliyopita alilia kwa hasira baada ya Ureno kupoteza mechi ya fainali ya Ulaya 2004 ‘Euro 2004’ katika mechi ya fainali dhidi ya Ugiriki.

Ni kama vile alipata fursa ya kujikumbusha chozi la miaka hiyo na kujikuta akiwa mwingi wa furaha.

Ni hatua ya kipekee kwa mchezaji huyo ambaye alifunga mabao 17 katika msimu wa 2013/14 rekodi ya kipekee ya Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya kucheza katika mechi 11 kati ya 13.

Baada ya kumzungumzia huyo, ukija kwa Messi rekodi yake ya Ligi ya Mabingwa mwaka uliofuata yaani msimu wa 2014/15 ulimfanya awe mfungaji bora mwenye mabao mengi katika mashindano hayo, mabao 77, akiwa amemzidi Ronaldo kwa bao moja. Lakini kama itatoke kwa Messi kutakiwa achague jambo la kuvutia katika msimu huo na pengine katika maisha yake yote ya soka hapana shaka itakuwa ni Jumamosi ya Juni 6, 2015.

Ni saa 2:45 usiku kwenye Uwanja wa Olympia mjini Berlin, Barca wanaumana na Juventus katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, haukuwa usiku wa Messi kufunga mabao bali hakuna shaka kwamba ndiye aliyekuwa kichocheo na alikuwa na mchango wake mkubwa tu katika mabao yote matatu.

Alitawala mchezo licha ya ukweli kwamba kila mara alipogusa mpira kundi la wachezaji wa Juventus lilimzunguka kwa nia ya kumdhibiti. Bao la kwanza lilifungwa na Ivan Rakitic katika dakika ya nne, ni bao la tatu kufungwa kwa kasi katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Lakini Juventus wakapata bao lao baada ya mapumziko, walisawazisha katika dakika ya 55.

Katika dakika 10 zilizofuata walitawala mchezo, waliwatia presha wapinzani wao huku mchezo ukiendelea kuwa wenye ushindani.

Itaendelea Jumamosi ijayo