Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Coastal Union yaichapa Mwadui, mengine ndio hivyo!

Muktasari:

  • Ligi Kuu Bara imeendeleo leo Jumatatu ya Oktoba mosi kwenye viwanja sita.

Tanga. Kikosi cha Coastal Union ya Tanga kimeichapa Mwadui FC bao 1-0, kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Mkwakwani mkoani Tanga.

Coastal union ilipata bao la kuongoza dakika 36, lililodumu hadi mwisho,  likiwekwa wavuni na Deogratius Anthony aliyeunganishiwa pasi ya Hassan Ali.

Timu hiyo maarufu kwa jina la Wagosi wa Kaya ilicheza kwa nguvu na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara kupitia kwa washambuliaji wake Deogratius, Ayoub Lyanga na Hajji Ugando.

Kikosi cha Coastal kilikuwa na Hussein Sharifu 'Casilas' , Mbwana Hamis, Adeyum Salehe, Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Amme, Hassan Ally, Issa Abushehe, Mtenje Albano, Deogratius Anthony, Ayoub Lyanga na Hajji Ugando.

Mwadui FC kipa ni Arnold Massawe, Revocatus Mgunda, Miraji Mussa, Iddi Mobby, Joram Mgeveke, Jean Marie Girukwishaka, Leonard Ernest, Abdallah Sesame, Charles ilanfya, Ibrahim Nasser na Aalim Aiye.

 

MATOKEO YA TIMU NYINGINE

Singida United 1-0  Lipuli FC

Mtibwa Sugar 2-1 Biashara United

Ruvu Shooting 1-0 Mbao FC

Stand United  0 - 2 Mbeya City

JKT Tanzania 1-0 African Lyon