Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Coastal Union, Mwambusi wamalizana

MWAMBUSI Pict

Muktasari:

  • Habari hiyo imekuja siku moja kabla ya timu hizo kukutana kwenye Uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge, Dar es Salaam.

TAARIFA kutoka ilipo kambi ya Coastal Union, zinasema mchezo wao wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Jumatatu hii dhidi ya Yanga, kikosi hicho hakitaongozwa na kocha mkuu, Juma Mwambusi.

Habari hiyo imekuja siku moja kabla ya timu hizo kukutana kwenye Uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge, Dar es Salaam.

Mwanaspoti limetonywa, uongozi wa Coastal Union umemalizana na Mwambusi kutokana na matokeo mabaya iliyonayo timu hiyo tangu akabidhiwe.

Mwambusi alijiunga na Coastal Union Oktoba 23, 2024 akichukua mikoba ya David Ouma raia wa Kenya, hivyo amekaa kwa takribani siku 165 hadi Aprili 6, 2025. Kabla ya Mwambusi, kikosi hiko cha Wagosi wa Kaya kilikuwa chini ya Joseph Lazarao ambaye alikaimu kwa muda.

Chanzo cha kuaminika kutoka Coastal Union kimeliambia Mwanaspoti wamefikia muafaka wa kuachana na kocha huyo kutokana na matokeo Mabaya.

“Ni kweli tumemalizana na kocha Mwambusi kwa makubaliano maalumu na hatakuwa sehemu ya mchezo hapo Jumatatu kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu, tunaamini ni uamuzi sahihi tulioufanya,” kilisema chanzo hicho.

Mwanaspoti lilimtafuta Katibu Mkuu wa Coastal Union, Omar Ayoub na alisema hayupo kwenye nafasi nzuri kulizungumzia hilo kwa sababu yupo kikaoni.

“Nipo kikaoni siwezi kuzungumzia suala hilo kwa sasa,” amesema kiongozi huyo.

Mwenyekiti wa klabu hiyo, Muhsin Ramadhan Hassan alithibitisha taarifa hizo na Mwambusi aliitwa Tanga kwa ajili ya kujadili hatma yake na taarifa zingetolewa jana.

“Ni kweli Mwambusi aliitwa Tanga kwa ajili ya kuzungumzia mwenendo wa timu na kufikia makubaliano na taarifa itatolewa rasmi leo (jana).”

Kabla ya mchezo uliopita ambao Coastal ilifungwa 2-1 na Kagera Sugar ugenini, timu hiyo ilikuwa haijatikisa nyavu za wapinzani wake katika mechi sita mfululizo.

Mara ya mwisho kwa Coastal kufunga bao ilikuwa Februari 7, 2025 iliposhinda 2-1 dhidi ya JKT Tanzania.

Baada ya hapo, matokeo yalikuwa hivi; Mashujaa 0-0 Coastal, Pamba Jiji 2-0 Coastal, Coastal 0-0 Azam, Namungo 0-0 Azam, Coastal 0-3 Simba na Dodoma Jiji 0-0 Coastal.

Tangu akabidhiwe mikoba ya kuinoa Coastal Union, Mwambusi amekiongoza kikosi hicho katika mechi 15 za Ligi Kuu Bara, akishinda tatu, sare saba na kupoteza tano. Timu hiyo iliyocheza mechi 24 za ligi msimu huu, imekusanya pointi 25.