Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Benchi la Yanga wazawa watupu

Muktasari:

  • Mchezo huo ambao upo mapumzikoni kwa sasa huku timu hizo zikiwa hazijafungana, wachezaji waliokuwa benchi kwa upande wa Yanga ni, Metacha Mnata, Kibwana Shomari, Nickson Kibabage, Mudathir Yahya, Shekhan Ibrahim, Farid Mussa, Denis Nkane, Zawadi Mauya na Clementi Mzize.

KIKOSI cha Yanga kiko uwanjani muda huu kwenye Uwanja wa Azam Complex kucheza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji, ila jambo la kushangaza au kufurahisha katika benchi la timu hiyo hakuna mchezaji wa kigeni kwani wote ni wazawa.

Mchezo huo ambao upo mapumzikoni kwa sasa huku timu hizo zikiwa hazijafungana, wachezaji waliokuwa benchi kwa upande wa Yanga ni, Metacha Mnata, Kibwana Shomari, Nickson Kibabage, Mudathir Yahya, Shekhan Ibrahim, Farid Mussa, Denis Nkane, Zawadi Mauya na Clementi Mzize.

Yanga ambao ndio mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara wanaingia katika mchezo huu ikihitaji ushindi ili kurudisha kwenye mbio za kuwania ubingwa baada ya kulazimishwa suluhu mechi iliyopita dhidi ya Kagera Sugar Februari 2, Uwanja wa Kaitaba Bukoba.

Hata hivyo, licha ya Dodoma Jiji kukaza hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza ila rekodi zinaonyesha kikosi hicho tangu kipande rasmi Ligi Kuu Bara msimu wa 2019/2020 hakijawahi kuifunga Yanga kwani kimefungwa mara tano na kutoa sare moja.

Mchezo wa mwisho kwa timu hizo kukutana ulipigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi Mei 13, mwaka jana na Yanga ilishinda kwa mabao 4-2, huku mechi hiyo ikikumbukwa zaidi kwani ndiyo iliyowapa ubingwa rasmi wa 29 wa Ligi Kuu Bara.