Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bao la Ronaldo laitibulia Barca Nou Campa

KATIKA toleo lililopita mwandishi Luca Caioli alizungumzia bao tamu la Ronaldo alilofunga nchini Ureno wakati huo akiichezea Man United iliyokuwa ikiumana na FC Porto, bao hilo lilimfanya atwae tuzo ya Fifa ya Puskas ambayo hakuitarajia. Endelea…

“Sikutarajia kushinda chochote leo,’’ alisema Ronaldo baada ya hafla ya kukabidhiwa tuzo hiyo. Miaka kadhaa baadaye bao hilo hilo lilitajwa katika mabao bora sita katika hafla ya miaka 60 ya Uefa.

Ingawa kama ungemuuliza Ronaldo bao gani analoweza kulitaja kuwa ndio bora katika maisha yake ya soka, lisingekuwa hili.

Ronaldo: Barca v Real Madrid

Mechi hii ilichezwa Aprili 21, 2012 ilikuwa ni ya Ligi Kuu Hispania au La Liga msimu wa 2011/12. Ni bao ambalo lina thamani ya taji la La Liga.

Ni saa 2:00 usiku kwenye dimba la Nou Camp, ni mara ya kwanza tangu msimu wa La Liga wa 2008/09 Real walikuwa mbele ya Barca kuanzia mwanzo hadi mwisho, kwenye msimamo wa ligi walikuwa na pointi nne kuizidi Barca ya Pep Guardiola. Pointiii 85 kwa 81.

Ni pointi ambazo zilitosha kuwapa taji la La Liga nyumbani kwa mahasimu wao na kuizuia kasi ya Barca ya misimu mitatu.

Kama ilivyo kawaida, macho na masikio ya mashabiki yalikuwa kwa Messi na Ronaldo zaidi kuliko Real Madrid na Barca. “Mbio za taji la La Liga hazikuwa dhidi ya timu mbili, bali ilikuwa ni kati ya wachezaji wawili.” Lilieleza gazeti la michezo la Barca.

Na ndio maana haikuwa vigumu kuona namna ambavyo Ronaldo na Messi wamezipaisha timu zao kwa hatua hiyo kwa kipindi hicho.

Katika mechi 32 za La Liga kila mmoja amefunga mabao 41, hiyo ni rekodi ya Ronaldo ya msimu wa 2010/11, “hakijawahi kuonekana kitu kama hicho, La Liga haijawahi kuwa na wachezaji wa kiwango cha juu wawili kama hao,’’ lilichambua gazeti hilo.

Ukiachana na fainali ya Kombe la Mfalme mwaka 2011, Ronaldo ni kama alipotea hivi kabla ya kurudi kwa kasi hadi aliporudi na kuwa anapambana ana kwa ana na Mess, ilikuwa hivyo akiwa United na hata akiwa Real Madrid, rekodi ni hizo hizo.

Katika tukio hilo habari ni tofauti kama ilivyojionyesha kuwa ya kipekee, alifunga bao la ushindi lililoifanya Real Madrid ya Mourinho ikapata ushindi wa mabao 2-1 na kuongoza kwa pointi saba dhidi ya mahasimu wao Barca, ushindi uliotosha kuwahakikishia taji.

Bao hilo lilipatikana katika dakika ya 73 muda mfupi baada ya Barca kupata bao la kusawazisha lililofungwa na Alexis Sanchez, walivunja mpango wa Barca kutaka kufanya shambulizi la kushtukiza.

Mesut Ozil aliunasa mpira kutoka kwa Di Maria mbele kidogo ya eneo la kati na kupiga krosi iliyokwenda kwa Ronaldo, aliambaa na kumuacha Mascherano huku akimsogelea kipa wa Barca, Victor Valdes, aliupeleka mpira kulia na kumshinda Valdes aliyekuwa karibu na mwamba wa goli.

Ni shuti la maana lililozaa bao ambalo alilishangilia kwa kukimbia katika eneo la mashabiki wa Barca, kama vile akiwataka kutulia, akiiga staili ambayo Raul, mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid aliwahi kuifanya.

“Tulieni tulieni, niko hapa,’’ alisema kwa sauti ya ju, akiwa anajua nini maana ya bao hilo.

Katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mechi hiyo Ronaldo alisema, “ni bao muhimu lakini ushindi wa timu kwa jumla ni kitu muhimu,” alikuwa amefunga bao kwa mara nyingine Nou Camp, akifanya kazi yenye manufaa iliyofuta ukame wa miaka mitatu kwa timu yake.

Na kwa namna vyombo vya habari vya Madrid vilivyolichukulia tukio hilo, ilikuwa kama vile Ronaldo alimbwaga Messi.

Itaendelea Jumamosi