Azam yaitangulia Mtibwa Sugar Manungu

Saturday May 21 2022
Azam PIC
By Olipa Assa

LICHA ya Azam FC kuongoza kwa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao Mtibwa Sugar, dakika 45 za kipindi cha kwenye uwanja wa Manungu Complex.

Bao la Azam FC limefungwa na Ayubu Lyanga dakika 20 ni kama lilichochea morali kwa wachezaji wa timu hizo kuongeza kasi ya mchezo na kushambuliana kwa zamu.
Dakika chache baada ya bao, hilo wachezaji wawili wa Mtibwa Sugar,walilimwa kadi za njano,kipa Jeremiah Kisubi aliyekuwa anabishana na refa kutokana na Ibrahim Erika kufunga bao la mkono naye akaadhibiwa.

Zilikuwa dakika 45 ngumu ndani ya uwanja, ila tamu kwenye macho ya mashabiki waliokuwa wanaitazama mechi hiyo, jinsi ambavyo wachezaji walijitoa kutetea timu zao.
Azam FC inasaka nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara,endapo ikishinda mchezo wa leo itafikisha pointi 36 itaishusha Geita Gold yenye pointi 34, wakati Mtibwa Sugar ikifanikiwa kunyakua pointi haitapanda zaidi ya kufikisha alama 31 sawa za KMC.

Advertisement