Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Athari za kubeti, shisha zaishtua Serikali, sheria zake kupitiwa upya

Muktasari:

  • Kauli hiyo ya Serikali inakuja wakati kukiwa na wimbo la kuvunjika kwa ndoa na wahusika kudai talaka.

Serikali imetoa wito kwa jamii na taasisi zilizopewa dhamana ya kufungisha ndoa pamoja na wazazi na walezi kuhakikisha wanaendelea kutoa elimu ya maadili kwa wanandoa.

Kauli hiyo ya Serikali inakuja wakati kukiwa na wimbo la kuvunjika kwa ndoa na wahusika kudai talaka.

Akiwasilisha makadirio ya mapato ya Wizara ya Sheria na Katiba kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Waziri Dk Damas Ndumbaro, amesema wazazi na walezi hawana budi kuongeza kasi ya kutoa elimu ya maadili ya ndoa.

Dk Ndumbaro amesema katika kipindi cha Julai, 2024 hadi Aprili, 2025, Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) umesajili na kutoa vyeti 675 vya talaka sawa na asilimia 116 ya lengo la kusajili talaka 583.

“Natoa wito kwa viongozi wote waliopewa dhamana ya kufungisha ndoa, wazazi na walezi kuendelea kutoa elimu ya maadili kwa wanandoa,” amesema.

Amesema takwimu hizo ni kubwa na kwamba, wanandoa hawana budi kujenga utamaduni wa kuvumiliana na kutatua changamoto zinazojitokeza kwa njia ya majadiliano ili kupunguza talaka ambazo zinaathiri malezi ya watoto kwa mustakabali wa haki zao.

Dk Ndumbaro amesema katika kipindi cha Julai, Pia, amesema kwa mwaka 2024 hadi Aprili, 2025, Wakala umesajili marejesho ya shahada za ndoa 35,052 zilizofungwa sawa na asilimia 65 ya lengo la kusajili ndoa 54,167.

Aidha, amesema jumla ya leseni mpya 2,994 za kufungisha ndoa zilitolewa kwa viongozi wa dini na leseni 986 za kufungisha ndoa zilihuishwa.
Mbali na hilo, Dk Ndumbaro amesema katika kipindi husika nakala ngumu 233,514 za ndoa zimehifadhiwa katika mfumo wa kielektroniki.