Aisee 20 Pacent amtaja Bobani
MSANII 20 Pacent kumbe sio mtu wa kufuatilia mistari ya nyimbo tu, jamaa anafuatilia na vipaji vya soka pia.
Akizungumza na Mwanaspoti hivi karibuni alisema: “Ukifanya uchunguzi wa wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu vya soka nchini, utabaini kwamba ni wachache na wanatumika kwa muda mrefu kama wakati wengine kama si kugeukia shughuli nyingine basi wengi wao wapo madaraja ya chini.
“Achilia mbali ushabiki, mtu kama kiungo Haruna Moshi ‘Boban’ leo asingekuwa anacheza madaraja ya chini, tungekuwa tunamsikia nje ya nchi, lakini ukifuatilia kwa nini anashindwa kudumu kwenye ligi kuu, utabaini kwamba ana msimamo wa kulinda haki za kazi yake.
“Wakati mwingine, haki inaweza kuchelewesha maendeleo ya mtu kwani unapokuwa unatofautiana na kundi la watu wengi unaonekana siyo na wakati mwingine unasemewa vitu tofauti, lakini ndiyo maisha lazima kuishi kwa ujasiri na kukubaliana na hali halisi unayokuwa nayo.”