Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

30 wahitimu stashahada ya ukocha Arusha

Jumla ya makocha 30 wamefanikiwa kuhitimu mafunzo ya ukocha ngazi ya stashahada ya shirikisho la soka Afrika daraja D (CAF diploma D) yaliyofanyika Kwa siku 10 mkoani Arusha.

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)  yametolewa na mkufunzi ngazi ya CAF, Fikiri Elias Kwa lengo la kuwapandisha madaraja makocha wa chipukizi wa ngazi za chini.

Akizungumzia mafunzo hayo, Katibu wa Soka  Arusha, Emmanuel Anthony alisema mafunzo hayo ni muendelezo wa kozi za kuongeza wigo wa makocha wa watoto chipukizi nchini wenye weledi wa mpira wa miguu hasa kuibua na kuendeleza vipaji vya watoto wadogo wenye kujua Sheria za soka, nidhamu na kuwa mabalozi wazuri kimataifa.

"Lengo la mafunzo haya ni kuwa na makocha wengi wenye ujuzi wa kuibua vipaji vya mpira wa miguu vya watoto wetu Kuanzia mtaani na kuviendeleza tena wenye nidham na weledi, hii itatusaidia kutumia rasilimali soka iliyopo ndani ya watoto Kwa manufaa ya nchi hasa katika Mashindano mbali mbali ya vijana watakaowakilisha kimataifa"

Naye mkufunzi wa mafunzo hayo Elias, alisema kuwa Kwa muda wa siku 10 wamefanikiwa kuwajengea uwezo na msingi mpya makocha hao 30 kwa ajili kuibua na kufundisha vijana wadogo wa mpira wa miguu Kuanzia miaka 8 hadi 18.

"Tumewafudisha mengi na kuwasisitiza zaidi kujua misingi ya ukocha, kanuni na taratibu za mwalim akiwa uwanjani,  anatakiwa kufanya Nini na zaidi tumewapa mbinu ya jinsi ya kundaa  mpango kazi wake wa ufundishaji wa mwezi pia kutengeneza utimamu wa mwili wa mchezaji wake, lishe na mda wa mapumziko"

Kocha Elias alitumia nafasi hiyo kuwataka makocha wahitimu wakafanyie kazi mambo yote waliyofundishwa Ili waweze kunuifa na kazi yao na zaidi kuwa msaada Kwa mpira wa Tanzania wenye uhaba mkubwa wa wachezaji vijana wenye vipaji na nidhamu uwanjani.

Nae mmoja wa washiriki wa mafunzo, Wilson Shelukindo alisema kuwa wamejifunza mengi katika mafunzo hayo na kuwajengea ufahamu na umuhimu wa kuibua vijana na kuwaendeleza Kwa kuzingatia misingi, weledi na nidhamu binafsi ya mchezaji.

"Mimi binafsi naenda kwetu Lushoto kuhakikisha nawaibua vijana wengi wacheze mpira hasa wasichana ambao wamekuwa na fursa nyingi katika soka la nchi yetu"

Thomas Mbawe aliiomba TFF kufanya mafunzo hayo mara Kwa mara na itakuwa na manufaa makubwa ikiwemo kufahanu umuhimu lishe, na chakula, lakini nidham inavyoweza kumsaidia mchezaji na zaidi kupatikana makocha wenye elimu ya kufundisha soka na sio uzoefu pekee.