Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

#TBT ZILITRENDI: Micho awatimua makomandoo Yanga

#TBT ZILITRENDI: Micho awatimua makomandoo Yanga

KAMA kawaida tunaendelea na zile zilizotrendi miaka ya nyuma na leo tunaenda hadi Machi 3, lakini mwaka 2007.
Siku hiyo buana iliripotiwa tukio la aliyekuwa Kocha Mkuu Mpya wa Yanga, Sredejovich Milutin ‘Micho’  kuamua kuwatimua makomandoo wa klabu hiyo.
Micho anafahamika kwa misimamo yake mikali na siku hiyo, aliwaonyesha jinsi alivyo baada ya bosi huyo wa benchi la ufundi kuamuru makomandoo hao washushwe kwenye basi lililokuwa limewabeba wachezaji.
Hali hiyo iliwaacha midomo wazi baadhi ya mashabiki wa Yanga kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam saa 1 usiku, dakika chache kabla ya basi lililokuwa limebeba wachezaji hao ili kuwapeleka kambini kwenye Hoteli ya Landmark baada ya kumaliza mazoezi yao.
Baada ya wachezaji kupanda kwenye basi hilo aina ya Toyota Coaster na kutaka kuondoka, Micho ambaye hutumia usafiri binafsi alichungulia dirishani na kuwaona makomandoo hao kama sita hivi.
Papo hapo akaamuru dereva kusimamisha gari haraka na kwamba kuna kitu kibaya kimetokea.
Micho alimwita kiongozi mmoja wa Yanga, Abdul Sauko kwa sauti kubwa na kumwambia bila woga hataki kuwaona makomandoo kwenye gari hilo na kuwataka wateremke haraka.
“Sauko...hilo gari ni kwa ajili ya wachezaji, sitaki kuwaona hao wanaoitwa makomandoo...waambie washuke wakapande teksi..hilo gari ni kwa ajili ya wachezaji tu,” alisema kocha huyo kwa hasira akifuta utamaduni wa kizamani wa makomandoo kupanda gari la wachezaji kwenda au kutoka uwanjani.
Baada ya kauli hiyo, makomandoo hao hawakushuka mara moja wakisubiri mazungumzo ya faragha yaliyokuwa yakiendelea pembeni baina ya Sauko na Micho, lakini baada ya kuona Mserbia huyo haelewi somo wakaanza kushuka mmoja baada ya mwingine na kutoka nje ya uwanja ili kupanda daladala.