Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba: Tulieni mtaelewa tu

MDOGO mdogo, mtatuelewa tu. Ndio kauli ya mashabiki wa Simba baada ya jana kushinda 1-0 dhidi ya Mbeya Kwanza na kupunguza tofauti ya pointi dhidi ya vinara Yanga kufikia tano, licha ya Wanajangwani kuwa na mechi moja mkononi.

Clatous Chama alifunga bao lake la kwanza tangu arejee Msimbazi akitokea RS Berkane ya Morocco, akimalizia piga nikupige iliyotokea kwenye lango la Mbeya Kwanza katika dakika ya 80, bao ambao haya hivyo lilipingwa sana na wachezaji wa timu hiyo Mbeya wakidai Medie Kagere alikuwa ameotea kabla ya mpira kumfikia mfungaji.

Kocha wa Mbeya City, Maka Mwalwisi alilalamikia bao hilo, lakini alichagua maneno ya kuongea pengine kukwepa rungu la Bodi ya Ligi, akisema: “Tumecheza vizuri, wachezaji wamefuata maelekezo vizuri kwa asilimia 90, tumecheza kwa kuwaheshimu, kwa kuwakabia kuanzia katikati, lakini tafsiri ya sheria imetuadhibu. (huku akirudia kwa zaidi ya mara tatu neno ‘tafsiri ya sheria imetuadhibu).”

Bao la jana limezua utata ikiwa ni siku tatu tu tangu Simba ishinde 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons kwenye uwanja huo huo wa Mkapa, kwa bao la penalti ya utata ambayo imelalamikiwa sana.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ ametamba kuwa wataendelea kupunguza pointi za watani zao Yanga na hatimaye kukaa kileleni.

Hadi sasa Yanga ndiyo inayoongoza kwenye msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 36 huku Simba ikishika nafasi ya pili kwa pointi 31.

Jumapili ijayo, Simba watakuwa nyumbani kucheza mechi ya kwanza hatua ya makundi ya Shirikisho dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast huku wakiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri. Baada ya hapo, Simba watakwenda Niger kucheza mchezo wa pili dhidi ya USGN. Simba hawatarejea nchini bali wataunga moja kwa moja Morocco kukamilisha mechi za hatua ya makundi mzunguko wa kwanza dhidi ya RS Berkane na wameamua kufanya hivyo ili kupunguza gharama kwani nchi hizo mbili zipo karibu.

Try Again alisema wapenzi na mashabiki wa timu hiyo wasiwe na wasiwasi katika mashindano yote matatu wanayoshiriki kwani watafanya vizuri.

Alisema anatambua mashabiki walikuwa na presha kubwa kwenye ligi baada ya kuona wapo awali walipitwa kwa pointi 10 dhidi ya watani zao lakini viongozi watahakikisha wanaandaa kikosi chao ili kufanya vizuri na kupunguza pointi hizo ikiwezekana kurudi kileleni mwa msimamo.

Wachezaji wa Simba walipewa mapumziko ya saa kadhaa na leo Jumatatu, wataendelea na mazoezi jioni ya kujiandaa na Asec.