Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyie! Kiiza hajaisha mjue

HUKO Kagera Sugar mzuka umerejea baada ya timu hiyo kupata saini ya mshambuliaji Hamis Kiiza ‘Diego’ kutoka klabu ya Proline FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Uganda.

Kocha mkuu wa kikosi hicho, Francis Baraza alisema ujio wa Kiiza ni pendekezo lake kwa ajili ya kutibu changamoto ya eneo la ushambuliaji na staa huyo hajaisha kama mashabiki wengi wanavyodai mitandaoni.

“Nina vijana wengi ambao bado wanaendelea kujifunza, naamini uzoefu wa Kiiza utaongeza chachu na morali ya wachezaji waliopo,” alisema na kuongeza:

“Mapumziko ya wiki mbili yamenipa mwanga mzuri wa kukifanyia tathimini kikosi changu kabla ya kurejea kuendelea na michezo yetu inayofuata.”

Nyota huyo wa zamani wa Simba, Yanga amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuwatumikia ‘Wanankurukumbi’ akiwa mchezaji huru.

Mbali na usajili huo, Kagera Sugar pia imenasa saini ya mshambuliaji Fredy Cosmas ‘Balotelli’ kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Mwadui FC ambayo inashiriki Ligi ya Champioship.

Cosmas amewahi kuhudumu katika klabu kadhaa ikiwemo Bandari FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Kenya.