Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbao yaingia kimyakimya, Simba shangwe Kirumba

Muktasari:

Mbao iwapo itashinda mchezo huo itapanda hadi kukaa kileleni mwa Ligi Kuu Bara

T: Mbao yaingia kimyakimya, Simba shangwe Kirumba

S: Mbao iwapo itashinda mchezo huo itapanda hadi kukaa kileleni mwa Ligi Kuu Bara

Mwahiba Richard

Mwanza. Mbao FC imefika uwanjani saa 8:18 mchana ikiitangulia Simba iliyoingia saa 8:57 tayari kwa mechi yao itakayoanza saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Mashabiki wa Simba waliokaa eneo la vyumba vya kubadilishia nguo wachezaji waliishangilia timu yao kwa nguvu tofauti na ilivyoingia Mbao wenyeji, lakini ina mashabiki wachache.

Mbao iliongozwa na magari mawili madogo wakati Simba iliongozwa na gari la Polisi wa kuzuia ghasia (FFU). Timu zote zimeingia mlango mkubwa wa magari na kuingia vyumbani.

Hata hivyo, mpaka muda huu mashabiki ni wachache ingawa bado wanaendelea kuingia.

Vikosi

Mbao: Hashim Mussa, Vicent Philipo, Amos Charles, David Mwassa, Peter Mwangosi, Ally Mussa, Said Khamis, Hussein Seleman, Rajesh Kotecha, Pastory Athanas na Aboubakary Mfaume.

Benchi: Bruno Thomas, Hamimu Abdul, Yusuph Amos, Evarijestus Mujwahuki, Zamfuko Elias, Roland Msonjo na Emmanuel Mtumbuka

Simba: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Clatous Chama, John Bocco, Emmanuel Okwi na Mohammed Ibrahim

Akiba: Deogratius Munish, Paul Bukaba, James Kotei, Said Ndemla, Meddie Kagere, Marcel Bonaventure.

Waamuzi: Waamuzi: Mbao vs Simba Katikati: Jonesia Rukyaa (Kagera), R1: Makame Mdogo (Shinyanga), R2: Martin Mwalyaje (Shinyanga)