Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ligi Daraja la Kwanza yaanza kwa kishindo, Mbuni yatakata

Mbuni yatakata ikiinyuka Ndanda

Muktasari:

  • Mchezo huo ni wa kwanza wa ufunguzi wa Ligi Daraja la Kwanza (Championship) ambapo Mbuni imeanza vyema dhidi ya Ndanda ikiondoka na pointi tatu.

TIMU ya Mbuni FC imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wageni wao Ndanda FC kutoka Mtwara katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Mbuni imeibuka na ushindi huo katika mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa Ligi Daraja la Kwanza (Championship) iliyoanza leo September 17 katika viwanja mbali mbali mbali nchini.

Ilichukua dakika 28 pekee timu ya Mbuni kupata bao la ufunguzi baada ya mchezaji wake Ayubu Shabani kumpoteza kipa wa Ndanda, Samwel Brazio kuokota mpira nyavuni na kuwafanya kwenda mapuymziko dakika 45 za kwanza kwa kifua mbele.

Kipindi cha pili dakika ya kwanza tu, Mbuni walijipatia bao la pili kupitia mkwaju wa penati uliopigwa na mchezaji Yunus Hassan baada ya mchezaji Lucas Charles kufanyiwa madhambi eneo la hatari.

Dakika ya 90 mchezaji Yunus Hassan alipigilia msumari wa mwisho kwa shuti la mbali alilopiga kabla mwamuzi wa kati Walter Josephat Kutoka Pwani kupuliza kipenga kuashiria kumaliza mchezo katika dakika tatu za nyongeza.

Matokeo mengi ya Ligi Daraja la Kwanza (Championship) ni;
Mashujaa 1️⃣-1️⃣Transit
Kitayosce 1️⃣-1️⃣Pan African
A. Sports 1️⃣-1️⃣Green
Mbuni 3️⃣-0️⃣ Ndanda
Fountain 1️⃣-0️⃣ Biashara
JKT 2️⃣-0️⃣ Copco
Gwambina 1️⃣-2️⃣Mbeya Kwanza
Pamba 1️⃣-0️⃣KenGold.