Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huyo Ajibu ameshindikana aisee!

Muktasari:

  • Hata hivyo, mambo yapo ovyo, kama ambavyo Haruna Niyonzima waliyepishana naye anavyowasononesha mashabiki wa Msimbazi wakiamini walipigwa kwa kumtoa Ajibu ili wamsajili kiungo huyo Mnyarwanda.

KUNA Ibrahim Ajibu mmoja tu pale Yanga. Ndio, ni straika aliyesajiliwa kwa mbwembwe kutoka Simba msimu uliopita na mashabiki wa Jangwani walitarajia kuona makubwa kuliko aliyokuwa akiyafanya akiwa Msimbazi.

Hata hivyo, mambo yapo ovyo, kama ambavyo Haruna Niyonzima waliyepishana naye anavyowasononesha mashabiki wa Msimbazi wakiamini walipigwa kwa kumtoa Ajibu ili wamsajili kiungo huyo Mnyarwanda.

Sasa unaambiwa, Ajibu amekuwa akiwazingua mabosi wake kutokana na tabia yake ya kukacha mazoezi kila mara na kuwekewa utaratibu wa kukatwa Sh50,000, lakini kumbe wala jambo hilo halimshtui na anaendelea kama kawaiada.

Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh alifichua jambo kuhusu staa huyo baada ya kuona ana tabia ya kutega mazoezi waliamua kumpa adhabu ya kufyeka kiasi hicho cha fedha katika mshahara wake wakiamini labda itamrekebisha.

Hata hivyo, straika huyo anaendelea na mtindo huo, ambao uliwahi kulalamikiwa pia hata alipokuwa akikipiga Msimbazi kwa misimu mitatu mfululizo tangu alipopashindwa kutoka timu ya vijana.

“Ajibu tangu aliporuhusiwa tulivyotoka Rwanda kuumana na Rayon Sports hajajiunga tena na timu kwa mazoezi na wala hatuna taarifa zake kama ana tatizo ama la, ila alikuwa na taarifa ya mazoezi tangu jana (juzi),” alisema Hafidh.

Hafidh aliongeza mchezaji huyo wamejaribu kukaa naye na kumshauri juu ya suala hilo lakini haonyeshi kubadilika na kudai kuwa uongozi umeamua kumuacha kwani tayari hatua za kinidhamu wanaendelea kumchukulia. Mwanaspoti lilimsaka Ajib kufahamu kilichompata lakini hata hivyo simu yake haikuwa na majibu.

Juu ya maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Chama la Wana, Stand United utakaochezwa jijini Dar es Salaam wiki mbili zijazo, alisema wamepania kuzoa pointi zote tatu.

Alisema mazoezi yao yanayoendelea kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini yapo sawa japo idadi ya majeruhi imeongezeka.

“Leo (jana) tulikuwa na idadi ndogo ya wachezaji kutokana na ongezeko la majeruhi, mfano Heritier Makambo, Juma Mahadhi, Amissi Tambwe, Yusuf Mhilu, Said Mussa, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Juma Abdul na Ramadhani Kabwili walishindwa kujumuika na wenzao.”

Kuhusu Makambo alisema alishindwa kufanya mazoezi kwa vile alichanika nyama za paja katika mchezo wao dhidi ya Rayon, ila anaweza kuwepo dhidi ya Stand.