Tanzania imemaliza kwenye nafasi ya tatu katika matokeo ya jumla kwa vijana chini ya miaka 20 mashindano ya riadha Afrika ya kanda.
Mashindano hayo ya siku mbili yamefungwa jioni hii kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Ethiopia imetawazwa kuwa mabingwa wa jumla baada ya kuvuna medali sita, tano za dhahabu na fedha moja.