Baada ya kuteswa kwa misimu mitatu mfululizo, hatimaye leo Prisons imekataa unyonge kwa Azam baada ya kuwanyoosha bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Mara ya mwisho Prisons kushinda mbele ya Azam ilikuwa April 2, 2019 waliposhinda 1-0 kwa bao la Jumanne Elfadhil dakika ya 36 na leo wanatakata tena baada ya ukame wa muda mrefu.