Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ufalme wa Yanga umepita na hawa Simba SC

UFALME Pict


KATIKA soka la Tanzania, furaha ya mashabiki wa Yanga ni kuwaona watani zao wa jadi Simba wakitekeseka. Upande mwingine, Simba nao wanafurahi kuona Yanga ikitaabika.


Kwa sasa tukiwa msimu wa 2025-2026, ubao unasoma 1-1 kati ya watani hao wa jadi baada ya wababe wa Jangwani kufikia rekodi iliyowekwa na Wekundu wa Msimbazi kwa kutwaa mataji manne mfululizo ya Ligi Kuu Bara.


Yanga imefanya hivyo baada ya kutawala kuanzia msimu wa 2021-2022 hadi 2024-2025 ambapo imetwaa taji la Ligi Kuu Bara huku Simba ikiambulia patupu.

Kabla ya hapo, Simba nayo ilibeba mara nne mfululizo ambayo ni 2017-2018, 2018-2019, 2019-2020 na 2020-2021.

Msimu huu wa 2025-2026 ukiwa unaendelea huku Yanga ikiwa na Ngao ya Jamii ikitwaa mbele ya watani zake, Simba, inatafuta rekodi ya kutwaa taji la tano mfululizo la Ligi Kuu Bara ikiwa na kocha mpya, Romain Folz.

Wakati Yanga ikipambania rekodi hiyo, Simba pia haitaki unyonge tena kutokana na kusajili wachezaji sambamba na kupambana kuunda benchi jipya la ufundi baada ya kufikia makubaliano ya kusitisha mkataba na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Fadlu Davids, aliyeondoka hivi karibuni.

Mwanaspoti inakuletea makocha saba waliopita Simba ndani ya misimu minne wakiokosa taji la Ligi Kuu Bara kuanzia 2021-2022 na sasa ina mpango wa kushusha kocha mwingine, huku Yanga ndani ya misimu hiyo ya mafanikio ikinolewa na makocha wanne.

Kwenye utawala huo Yanga imenolewa na Nasreddine Nabi ambaye aliipa Yanga mataji mawili ya ligi, Migueli Gamondi (taji moja), Sead Ramovic (hakuchukua akidumu takribani miezi miwili) na Miloud Hamdi aliyeipa ubingwa wa mwisho wa ligi.

Kocha Didier Gomes ndiye wa mwisho kuipa Simba taji la ligibmsimu wa 2020-2021 akiingia katikati ya msimu na kuondoka msimu ambao ndio Yanga ilioanza kutwaa mataji mfululizo hadi mwishoni mwa msimu uliopita.

UFA 05

PABLO FRANCO

Pablo Franco siku 204 alikaa Simba ambapo Novemba 7, 2021 ilimtambulisha akichukua mikoba ya Didier Gomes na hukudumu kwenye kikosi hicho kwani Machi 31, 2022 Simba iliachana na Mhispania huyo na nafasi yake kuchukuliwa na Zoran Maki aliyedumu kwa siku 67 kabla ya nafasi hiyo kukaimiwa na Juma Mgunda.

Itakumbukwa wakati Pablo akiwa Simba aliiacha timu hiyo kwa heshima akiifikisha hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, lakini ikatolewa na Orlando Pirates kwa matuta.

Kwenye hatua hiyo Simba chini ya Pablo mechi ya kwanza ilishinda bao 1-0, lililofungwa na Shomary Kapombe na ile ya marudiano Afrika Kusini Orlando ilishinda 1-0 ambapo mechi ilikwenda kwenye penalti Simba ikafungwa 4-3.

Msimu huo, Pablo alichukua taji la Mapinduzi huku mataji mengine yakichukuliwa na Yanga, ilhali kocha huyo raia wa Hispania akikabiliwa na majeruhi wengi katika kikosi chake.

Januari 13, Simba chini ya Pablo ilichukua ubingwa huo baada ya mchezo wa fainali kushinda bao 1-0 dhidi ya Azam kwa bao lililofungwa na Meddie Kagere.

UFA 02

JUMA MGUNDA

Juma Mgunda akiwa na Simba iliichapa Prisons bao 1-0 kwenye Ligi Kuu Bara ikiwa ni mara kwanza inaibuka na ushindi nyumbani kwa Prisons tangu 2019, ikaichapa Dodoma Jiji kwa mabao 3-0 kisha ikatoka sare ya 1-1 na Yanga.

Baada ya mchezo dhidi ya Yanga, Mgunda alikutana na kichapo cha kwanza alipolala 1-0 dhidi ya Azam, lakini kikosi chake kikarejea kwa nguvu na kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mtibwa kikiwa ni kipigo kikubwa kutolewa na Simba msimu huo.

Hapo kati timu hiyo ya Mgunda ilicheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Kipanga na kushinda 3-0 kisha ikashinda 1-0 dhidi ya Malindi.

Kwenye ligi katika michezo mitano timu hiyo ilifunga mabao 10 na kufungwa mawili na timu kubwa za Azam na Yanga, rekodi ambazo mashabiki wa Simba wanatakiwa kuzisubiri kwa sasa wakati timu hiyo itakuwa chini ya kocha mpya.

Mgunda akiwa na Simba aliweka rekodi ya kuwa kocha pekee mzawa kuipeleka timu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika tangu 1998 wakati huo ikiwa chini ya hayati Tito Mwaluvanda alipoifikisha Yanga kwenye hatua hiyo.

Mgunda alishinda michezo miwili baada ya kuichapa Big Bullets ya Malawi mabao 4-0, lakini akaichapa De Agosto ya Angola, jumla ya mabao 4-1. 

Pia aliweka rekodi ya kocha wa kwanza mzawa kuifikisha timu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza tangu 1998, alipoziondoa Nyassa Bullets kwa mabao 4-0, De Agosto kwa mabao 4-1.

UFA 01

ZORAN MAKI

Zoran Manojlovic maarufu kama Maki alidumu siku 67. Kocha huyo alimalizana na Simba baada ya makubaliano ya pande mbili na viongozi ikieleza alisitisha mkataba wake wa mwaka mmoja aliousaini pamoja na kocha wa viungo, Sbai Karim na wa makipa, Mohammed Rachid.

Kikosi hicho ambacho jana kilitarajiwa kucheza chezo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili dhidi ya Namungo jana katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kikiwa chini ya kocha msaidizi Selemani Matola huku mchakato wa kutafuta kocha mkuu ukiendelea.

Zoran aliiongoza timu hiyo kwenye michezo miwili akishinda yote akianza na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Geita Gold Agosti 17, 2022 kisha ushindi wa 2-0 kwa Kagera Sugar Agosti 20 mechi zote zikichezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Zoran mwenye uraia pacha wa Serbia na Ureno alitambulishwa kukinoa kikosi hicho Juni 28, 2022 akichukua mikoba ya Mhispania Pablo Franco aliyejiunga na Simba Novemba 10, 2021 kabla ya kutimuliwa Mei 31, 2022.

UFA 06

ROBERTO OLIVEIRA ‘Robertinho’

Robertinho alidumu siku 310. Kocha huyo alitimuliwa na Simba akiwa amepoteza mechi moja ya Ligi Kuu tangu alipojiunga nayo Januari 2023 ambapo aliiongoza katika mechi 17 za ligi ikishinda 14, sare mbili na kupoteza hiyo moja huku ikifunga mabao 42 na kuruhusu mabao 15.

Kocha huyo aliondoka akiiacha Simba na taji moja ambalo ni la Ngao ya Jamii msimu huo na pia akiiongoza kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliotangulia ambao pia aliifanya imalize katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

UFA 04

ABDELHAK BENCHIKHA

Benchikha alidumu Simba siku 149 akiicha ikiwa katika nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kukusanya alama 36 kwenye michezo 16.

Kocha huyo aliyeajiriwa na kutambulishwa na Simba Novemba 28 2023, aliiongoza kwenye mechi nane za Ligi Kuu Bara ikipoteza mchezo mmoja kama ilivyo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika alikoiongoza katika michezo mitano huku katika Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) Wekundu wa Msimbazi wakiwa chini yake walishuka uwanjani mara mbili.

Katika mechi hizo nane za Ligi Kuu Bara rekodi zinaonyesha Simba ilishinda mechi tano kutoka sare mbili na kupoteza mchezo mmoja ambao ni mbele ya Tanzania Prisons iliyowalaza kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro yote yakiwekwa kambani na nyota wa maafande hao Samson Mbangula.

Kwenye michezo ya CAF ambayo Simba ilitinga robo fainali kwa kishindo kupitia Kundi B ilipoteza mechi moja mbele ya Wydad CA ya Morocco, huku ikitoka sare mbili na kushinda mbili mbele ya Wydad na Jwaneng Galaxy ya Botswana waliyoifumua kwa mabao 6-0 na kufuzu robo fainali ikiwa ni mara ya nne katika misimu sita ya michuano ya klabu ya CAF.

Mechi mbili za ASFC, Benchikha aliiongoza timu hiyo kushinda zote ikianza kuinyoosha Tembo FC kwa mabao 4-0 katika hatua ya 64 bora na kufuzu 32 bora ambapo iliicharaza TRA Kilimanjaro kwa mabao 6-0 na kufuzu 16 bora.

UFA 03

FADLU DAVIDS

Licha ya kukosa ubingwa wa ndani, Fadlu aliifanya Simba kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Hiyo ilikuwa ni historia kwa timu hiyo baada ya miaka 31 tangu ilipocheza fainali ya mwisho katika michuano ya CAF.

Kwa miaka mingi chini ya makocha tofauti, Simba ilikuwa ikiishia hatua ya robo fainali.

Fadlu ambaye alidumu Simba kwa siku 444, amewaachia timu hiyo kibarua cha kufanya kwa viongozi ambao kwa sasa wanahaha kuhakikisha wanapata mrithi wake huku wakitekeleza mkakati wa muda mfupi kwa kumpa kazi ya muda mfupi kocha wa Taifa Stars, Hemed Suleiman ‘Morocco’ kuivusha hatua ya awali ya mzunguko wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika.


Kwa sasa timu hiyo ipo chini ya Matola.

UFA 07