Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Karibu tena Ligi Kuu Salum Mayanga

MAYANGA Pict

Muktasari:

  • Tathmini ya Kijiwe inaona kama Mbeya City haikutumia muda mrefu katika kulijadili jina la Mayanga na fasta tu ikaamua kumpa jukumu la kumalizia msimu na timu yao badala ya kwenda kwa kocha mwingine.

MIEZI michache tangu alipoachana na Mashujaa FC, Kocha Salum Mayanga amerejea tena Ligi Kuu safari hii akitua katika kikosi cha Mbeya City.

Tathmini ya Kijiwe inaona kama Mbeya City haikutumia muda mrefu katika kulijadili jina la Mayanga na fasta tu ikaamua kumpa jukumu la kumalizia msimu na timu yao badala ya kwenda kwa kocha mwingine.

Kuna sababu kama tatu hivi ambazo hapa kijiweni tunahisi zimechangia kwa kiasi kikubwa kuishawishi Mbeya City impe kazi Salum Mayanga ambaye mwanzoni mwa msimu huu aliinoa Mashujaa FC ya Kigoma.

Sababu ya kwanza ni nguvu kubwa na sauti ya mamlaka ambayo Mayanga anayo ndani ya chumba cha kubadilishia nguo cha Mbeya City na klabu hiyo kijumla.

Kabla hajainoa Mashujaa FC, Mayanga alikuwa ndiye Kocha Mkuu wa Mbeya City wakati huo ikiwa ligi ya Championship tena aliiacha ikiwa inakaribia kupanda Ligi Kuu.

Pia baadhi ya wachezaji wa Mbeya City walisajiliwa na yeye kipindi hicho kabla haijapanda daraja na baada ya kwenda Ligi Kuu bado wapo klabuni hapo hivyo hawatokuwa tayari kumwangusha.

Sababu ya pili ni uzoefu wake kwa soka na Ligi ya Tanzania. Ni miongoni mwa makocha wazawa waliofundisha kwa muda mrefu katika ligi yetu na hata timu ya taifa kwa nyakati tofauti.

Anazijua vyema tabia za wachezaji na namna gani ya kuishi nao hasa katika nyakati kama hizi ambazo timu inakuwa katika kipindi kigumu cha kupigania uhai wake kwenye ligi.

Kwa uteuzi wa Mayanga, Mbeya City wamefanya jambo sahihi pasipo kujali nini kitatokea mbele ya safari kama misheni itafanikiwa au haitofanikiwa.