Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shah Rukh Khan muigizaji tajiri namba moja duniani

KHAN PIct

Muktasari:

  • Hiyo ni mara ya kwanza kwa muigizaji huyo kuingia kwenye listi hiyo na anakadiriwa kuwa na utajiri wa rupia bilioni 124.9 ambazo ni sawa na Sh3.5 trilioni za Tanzania.

KWA mujibu wa ripoti ya Hurun India Rich List 2025, imetaja listi ya wasanii watano wenye utajiri mkubwa zaidi duniani na staa wa India, Shah Rukh Khan akiwa namba moja.

Hiyo ni mara ya kwanza kwa muigizaji huyo kuingia kwenye listi hiyo na anakadiriwa kuwa na utajiri wa rupia bilioni 124.9 ambazo ni sawa na Sh3.5 trilioni za Tanzania.

Staa huyo wa Bollywood amewazidi mastaa maarufu duniani kama Taylor Swift mwenye utajiri wa dola bilioni 1.3 ambazo ni sawa na Sh3.19 trilioni za Tanzania, Arnold Schwarzenegger (dola bilioni 1.2), Jerry Seinfeld (dola bilioni 1.2) na Selena Gomez (dola milioni 720).

Staa huyo aliyetamba kwa kuigiza kwenye nyimbo kama Kuch Kuch Hota Hai, Koi Mil Gaya, Tujh Mein Rab Dikhta Hai na nyinginezo, mara kadhaa ametajwa kwenye tovuti mbalimbali nchini India kuwa nyota mwenye utajiri mkubwa zaidi. 

KHAN 01

UTAJIRI WAKE
Mbali na kumiliki kampuni ya utayarishaji wa filamu ya Red Chillies Entertainment aliyoianzisha mwaka 2002, SRK pia anamiliki hisa kubwa katika timu ya kriketi ya Knight Riders Sports ambayo ni miongoni mwa timu maarufu na yenye mafanikio kibiashara nchini India.

Inaelezwa pia vyanzo vya utajiri wake vinatokana na nyumba za kifahari alizojenga ikiwemo ile ya Mumbai iliyoko Bandra, ikikadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya rupia bilioni 2 ambazo ni zaidi ya Sh60 bilioni za Kitanzania.

Anamiliki mali katika maeneo mengine ya kifahari kama Park Lane (London), Beverly Hills (Marekani) na nyingine zilizopo Dubai.

Mbali na nyumba pia anamiliki magari ya kifahari kama Bugatti Veyron yenye thamani zaidi ya Sh2 bilioni, Rolls Royce Phantom (Sh2 bilioni), Bentley Continental GT (Sh900 milioni) na nyinginezo.

KHAN 02

FILAMU MPYA
Kwa upande wa kazi, SRK yupo kwenye maandalizi ya filamu yake mpya King inayoongozwa na Siddharth Anand. Filamu hiyo inatarajiwa kumshirikisha pia binti yake Suhana Khan na wasanii wengine Abhishek Bachchan, Deepika Padukone, Rani Mukerji na wengineo
*****