Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MC Pilipili kuzikwa leo, wasanii wamlilia, Polisi wataja chanzo

Muktasari:

  • Shughuli ya kuuaga mwili wa staa huyo aliyekumbwa na mauti Jumapili itafanyika leo, huku wasanii mbalimbali wakiendelea kumlilia.

ALHAMISI ya leo huenda ikawa chungu zaidi kwa wakazi wa jiji la Dodoma hususani ndugu, jamaa na marafiki wa aliyekuwa mchekezaji nyota na mshereheshaji shughuli maarufu nchini,  Emmanuel Mathias ‘MC Pilipili’.

Shughuli ya kuuaga mwili wa staa huyo aliyekumbwa na mauti Jumapili itafanyika leo, huku wasanii mbalimbali wakiendelea kumlilia.

Jana mwili wake uliwasilishwa nyumbani kwao ambako waombolezaji wengi waliendelea kuonyesha upendo kwa kujitokeza kumuomboleza, lakini shughuli ya kuaga na kuzikwa kwa staa huyo inafanyika leo.

Mwili wa marehemu ulitarajiwa kuagwa na wanafamilia jana katika eneo la Swaswa na kulala hapo kabla ya leo kupelekewa kwenye viwanja vya Chinangali kwa Ibada Kuu na kutolewa heshima ya mwisho kitaifa na baada ya hapo kwenda kuzikwa kwenye makaburi ya Ipagala Kililo Kwanza kuhitimisha safari nzima ya miaka 40 ya MC Pilipili aliyezaliwa mwaka 1985.


AKUTWA NA MAJERAHA

Chanzo cha kifo chake bado kimeacha maswali, huku Jeshi la Polisi likibainisha kwamba staa huyo alishambuliwa kwani mwili wake umekutwa na majeraha katika sehemu mbalimbalimbali na wanaendelea na uchunguzi.

Kilichowasikitisha wengi ni kwamba taarifa hizo zinakuja wakati ambao wengi walikuwa wakimwona MC Pilipili alikuwa mtu aliyependa kufurahi wakati wote na wala kuwa na matukio ya kugombana na watu.

Pilipili anazikwa huku akiwaachia maswali si tu familia yake, bali hata mastaa wenzake ambao wengine wamefunguka namna walivyomfahamu na kufanya naye kazi wakieleza kwamba alikuwa ni mtu ambaye hakutaka kugombana na wengine.

Msemaji wa familia, Paschal Maingu, alieleza kuwa mwili wa marehemu ulikutwa na majeraha makubwa.

Paschal anasema kuwa, mdogo wa mwisho wa marehemu alimueleza kwamba, Pilipili alipitia mateso mazito kabla hajafariki.

Hali hii iliibua shaka kubwa ndani ya familia na jamii, huku uchunguzi wa polisi ukiendelea kutafuta chanzo halisi cha kifo hicho.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dk Ernest Ibenzi alisema MC Pilipili alipokewa hospitalini hapo akiwa tayari amepoteza maisha na mwili ulipelekwa hapo na wasamaria wema kati ya saa 10:30 na saa 11 jioni.

Baadaye kaka yake, Christopher Matebe, alithibitisha kuwa matokeo ya uchunguzi wa awali yanaonyesha kifo cha MC Pilipili kilitokana na kupigwa na watu wasiojulikana na familia ilihitaji uchunguzi wa kina.

Akiwa kwenye mahojiano na vyombo vya habari, alishukuru uongozi wa Hospitali ya General, pamoja na Mbunge wa Dodoma Mjini, kwa kuwa karibu na familia katika kipindi hiki kigumu.


HALI ILIVYO DODOMA

Dodoma ambako umauti ulimpata MC Pilipili, kuanzia Jumapili Novemba 16,2025 simanzi ilitanda hata katika mitandao ya kijamii kufuatia kifo cha msanii huyo.


RATIBA YA MAZISHI

Wakati uchunguzi ukiendelea, Kamati ya Mazishi imetoa ratiba kupitia Mwenyekiti John Mwangata (MC Mwangata), akisema kuwa ibada ya mazishi itafanyika leo Alhamisi, Novemba 20, kwenye viwanja vya Chilangali Park, Dodoma.

Hata hivyo, muda kamili wa ibada hiyo uliahidiwa kutangazwa baadae na inatarajiwa kuhudhuriwa na ndugu, majirani, wananchi wa Dodoma, pamoja na marafiki kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Baada ya ibada hiyo, maziko yatafanyika kwenye makaburi ya Ipagala yaliyoko Dodoma.


WASIKIE WASANII JB ATOA NENO

Mwigizaji mkongwe Jacob Steven ‘JB’,alisema kifo cha MC Pilipili ni kuvunjika kwa nguzo muhimu katika tasnia.

Anasema Pilipili alikuwa msanii aliyejua thamani ya kazi yake na ya wengine, alikuwa msikivu, mnyenyekevu na mtu wa kushirikiana bila makuu.

Pilipili hakutengeneza tu vichekesho, bali alitengeneza mazingira ya ushirikiano na upendo ambayo yalifanya sanaa kuwa sehemu salama kwa wengi.


SHILOLE NAYE

Msanii wa muziki, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ anamkumbuka Pilipili kama mtu wa watu na rafiki wa karibu wa wasanii wote bila kujali ukubwa wao.

Anasema kuwa, alikuwa na uwezo wa kuwatia moyo wengine hata katika nyakati ambazo naye alikuwa na changamoto zake binafsi.


WEMA SEPETU HUYU

Muigizaji Wema Sepetu, anasimulia namna Pilipili alivyoonesha upendo na ukaribu wa kweli hata nje ya kamera.

MKUDE SIMBA

Msanii Mussa Yusuf Mahenge ‘Mkude Simba’ alisema Pilipili alikuwa nguzo ya ushirikiano ndani ya ucheshi,

“Pilipili aliishi ucheshi kama huduma, sio kama kazi tu, alichekesha watu kama njia ya kuwapa faraja ya maisha.”