Jose Chameleone kuliamsha zilipendwa
Muktasari:
- Tamasha hilo, lililoandaliwa na Akibwoli Investments litafanyika kwenye Ukumbi wa Ndere Cultural Center, Uganda na linatarajiwa kuwapeleka mashabiki kwenye safari ya kukumbuka muziki, tamaduni na kumbukumbu za enzi za miaka ya 90.
MWIMBAJI mkongwe wa Uganda, Jose Chameleone amethibitishwa rasmi kwamba atakuwa miongoni mwa vinara wa tamasha linalosubiriwa kwa hamu la kukumbushia ngoma za zamani la ‘A Nite In The 90s’ litakalofanyika Desemba 6.
Tamasha hilo, lililoandaliwa na Akibwoli Investments litafanyika kwenye Ukumbi wa Ndere Cultural Center, Uganda na linatarajiwa kuwapeleka mashabiki kwenye safari ya kukumbuka muziki, tamaduni na kumbukumbu za enzi za miaka ya 90.
Usiku huo unatarajiwa kukumbushia ozoefu kamili wa mitindo ya zamani (retro), ukiwa na matembezi ya katika ‘red carpet’, eneo la kupiga picha, uwanja wa dansi, pamoja na madijei watakaopiga nyimbo kali zaidi za miaka ya 90.
Waliolipia tiketi pia watapata burudani ya bendi ya muziki, kipindi cha open mic, pamoja na vivutio vingine vingi vilivyoandaliwa ili kuufanya usiku huo kuwa wa kipekee na usiosahaulika.