Ile ya Gigy Money kumbe ni kiki tu!

Muktasari:
- Gigy alisema aliona kiki zake zimepungua mjini, ndo maana akaona azibusti ili apate kutrend.
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Gigy Money amefunguka na kusema hajafanya upasuaji wa makalio (Surgery) ili kuongeza shepu kama alivyosema wiki iliyopita bali ilikuwa ni kiki tu.
Gigy alisema aliona kiki zake zimepungua mjini, ndo maana akaona azibusti ili apate kutrend.
“Kila siku nawaambia Gigy ni kiki, sasa nimeona zilipungua mjini nikaona nifanye kiki ya kusema nimefanya Surgery ili tu ni busti kiki zangu mjini, sijatengeneza shepu wala makalio niseme tu ukweli,” alisema Gigy na kuongeza;
“Na nashukuru kiki yangu imekubalika si unaona navyozungumziwa, wapo watu wameamini na wengine hawajaamini ,na mimi nafanya kusudi nikotoka nanijaza mabox ili kuwachezesha watu akili zao, kufanya Surgery mchezo.”
Wiki iliyoisha kuna video ilisambaa ikimuonyesha Gigy Money akihojiwa akiwa kitandani na kusema anapata maumivu makali sababu ya kufanya Surgery ya kutengeneza shepu na makalio, ikiwa ni mfululizo wa kipindi cha maisha yake kinachorushwa na Zamaradi Tv.