Alikiba kudondosha ngoma mfululizo

Thursday June 10 2021
kiba pic
By Nasra Abdallah

Wakati wasanii wengi wakiwa wana tabia ya kuachia albamu zao kwa kuonyesha nyimbo zilizopo kwa msani Alikiba imekuwa tofauti
Hii ni baada ya leo Alhamisi Juni 10, 2021 kutambulisha wimbo wao  mpya wa ndombolo kutoka lebo ya Kings Music.
Wimbo huo ambao upo katika mahadhi ya bolingo, umewashirikisha wasanii wote waliopo katika lebo hiyo akiwemo yeye mwenyewe, mdogo wake Abdu Kiba, K2ga na Tommy Flavour.
Katika ujumbe wake akiwa anautumbalisha wimbo huo,Kiba amesema majira ya joto ndio haya itakuwa ni furaha, kwa kuangusha mziki mfululizo (Back 2 Back) mpaka pale albamu yangu itakapokamilika.
Hii itakuwa ni albamu yake ya tatu kuitoa ikitanguliwa na ile ya Cinderella na Ali K 4Real aliyoiachia mwaka 2008 ambayo ni miongoni mwa albamu kumi bora katika mtandao wa BOOMPLAY Afrika Mashariki.

Advertisement