Chirwa ataka bao la mapema kwa Dicha

Monday April 16 2018

 

By Khatimu Naheka

Awassa, Ethiopia. Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa amesema wanachotakiwa kufanya Jumatano dhidi ya Wolaitta Dicha ni kupata bao la mapema kwanza.

Chirwa alisema anataka kuona anawafunga mapema Dicha katika mchezo huo jambo litakalowachanganya wapinzani wao.

Mshambuliaji huyo aliyeukosa mchezo wa kwanza wa Yanga ikishinda mabao 2-0, alisema anaamini kikosi chao kitapangwa vyema kwa akili ya kutafuta ushindi na uwezo huo wanao.

"Nilikosa mechi ya kwanza, lakini nilisafiri na kuwahi kurudi ili niwaone mabeki wao, siyo wagumu sana najua kipi nikitumie ili niwafunge.

"Hii ni mechi ngumu nimejipangia kuhakikisha nafunga bao la mapema, tukifanikiwa hilo tunaweza kuwachanganya wapizani wetu na ushindi mkubwa utakuja,"alisema Chirwa.