RT yabariki Simbu kujitoa Madola

Tuesday January 9 2018

 

By Imani Makongoro


Dar es Salaam. Saa chache baada ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) kumpa ruksa Alphonce Simbu kushiriki mashindano yake binafsi, nyota huyo amesema hakuwa na nia mbaya kuomba aondolewe kwenye michezo ya Madola.

Katibu Mkuu wa RT, Wilhelim Gidabuday ameweka wazi kuwa Simbu hatokwenda kwenye Madola na badala yake atakwenda kwenye mbio za dunia za nusu marathoni za Machi nchini Hispania.

"Baada ya mbio hizo atakuwa huru kushiriki mbio zake binafsi hivyo hatokuwepo kwenye kikosi cha madola," alisema Gidabuday.

 Simbu alisema hana nia mbaya ya kutokuwepo kwenye timu ya madola.

"Sina nia mbaya isipokuwa mazingira yamenibidi iwe ivyo, nafarijika kuona nimesikilizwa na kupewa nafasi," alisema Simbu