Geay aenda kujisikilizia afya yake kwa Rais Trump

Monday May 14 2018

 

JAMAA kaamua. Mwanariadha Gabriel Geay ametimkia Marekani ili kucheki afya yake kwa madaktari maalumu ili akipanga kurejea katika mchezo huo aliojiweka nao kando kwa muda.

Geay aliondoka nchini siku chache baada ya kushindwa kumaliza Mbio za Ngorongoro Nusu Marathon, licha ya kuongoza kwa muda mrefu kabla ya kuishia njiani na kuwapisha Wakenya wang’are.

“Nitakaa huku kwa miezi mitatu nikiendelea kutazama afya yangu, huku nikishiriki mashindano madogomadogo ili kujiweka fiti zaidi kutokana na majeraha yaliyoniweka nje muda mrefu bila kushiriki mashindano makubwa maana.

“Nilipewa onyo la kutoshiriki mashindano hadi nitakapopona na kupata ushauri wa wataalam” alisema Geay.

Geay alipatwa na majeraha ya goti yaliyomweka nje zaidi ya miezi sita akiwa timu ya taifa akijiandaa na mashindano ya dunia ya Uingereza mwaka jana.