Ex wa Ronaldo adai CR7 si mbakaji

Muktasari:

  • Tuhuma za Ronaldo (33) kumbaka Mayorga (34) zimezidi kupamba moto katika siku za hivi karibuni tangu pale Jeshi la Polisi huko Las Vegas kudai hadharani kuwa limefungua jalada maalum la uchunguzi wa tukio hilo na iwapo mwanasoka huyo atakutwa na hatia, atachukuliwa hatua kali za kisheria. 

TURIN, ITALIA . SUPASTAA, Cristiano Ronaldo kwa sasa anatesa tu na penzi la mrembo, Georgina Rodriguez lakini demu wake mmoja wa zamani ameibuka na kusema yupo tayari kumtetea mwanasoka huyo maarufu kwenye kesi yake ya ubakaji.

Mrembo huyo wa Kihispaniola, Nereida Gallardo alisema kwa msisitizo kwamba Ronaldo sio mbakaji na atakuwa tayari kupanda kizimba cha mahakama kutoa ushahidi wa kumtetea mchezaji huyo.

Nereida alisema Ronaldo ni mwanamume safi, mwenye upande na siku zote amekuwa akiwajali wanawake wake.

Alisema: “Ni mwanamume lijali, anayependa na kuthamani. Hakika mara zote alikuwa mtu mwema kwangu. Ndio maana nilishangaa kusikia hizo habari za kubaka.” Nereida, ambaye alikuwa kwenye mapenzi na mwanasoka huyo kwa miezi minane aliongeza: “Cristiano alikuwa akinifanyia vizuri sana kwa muda wote tuliokuwa pamoja. Hajawahi kunishurutisha wala kukaribia kufanya hivyo. Sijawahi kuona akimlazimisha mtu. Na si mtu wa kutumia nguvu anapohitaji mambo ya chumbani.

Wawili hao waliachana Agosti 2008, miezi 10 kabla ya mrembo wa Kimarekani Kathryn Mayorga, kudai kutendewa tukio la ubakaji na mwanasoka huyo huko Las Vegas.