Tumevuna tulichopanda kwa madogo wa U-17

SAMTAIM kumchana mtu laivu sina noma, yaani kuwapa wana makavu sioni kwere wala nini? Ila kuna washkaji wanakuja inbobo na kunichimba biti, wakidai eti....ooh Mzee Baba we uzalendo huna...sijui mnazi wa Mnyamani, mara tumeshtukia we wa Kifusini...sio kwa michano yako ya kikuda!

Ishu zenyewe eti, kwa vile nimewahi kumpaka yule MC wa kule kwa Mnyamani pale alipozoza eti hata akija Barca ya yule Andunje wao...tena sio hii iliyowavuruga Manyumbu...eti ile ya Iniesta na Shavi ageini...Kuna wana povu liliwatoka, wakidai MC yupo freshi kisa tu, Mnyamani walimuotea Redi Devos pale neshno stadiamu kwenye zile ndiki za Kafu Championi Ligi!

Hata walipobanwa homu na Papa Fololo juzi kati alianza kuchonga tena, eti wanaenda kukinukisha awei na kumpiga mtu kwao...ila kila mmoko wenu, unajua kilichotokea, wana wamepigika kinoma! Ila nini sio ishu sana! Kila Mtizedi alijua mapema Mnyamani anaenda kupigika...kumng’oa Papa Fololo kwao, ilikuwa ni ishu, kwani si mnajua kuna Mmanga na ujanja wake alikula thamania pale...Ila kongole kwa wana wameipaisha neshno flagi, walipofika hata Kifusini wanapaota...unabisha nini sasa, wakati mara taraa wameingia grupu steji, lakini waligeuzwa wanyela buana! Washkaji waliwatumia Kifusini kama kapu lao la kuzoa mipointi, yaani ikienda awei kibano, ikija homu kisago...hata hapo mtabisha wakati K’Ogalo hapo kwa Presedaa msela, walipigika nje ndani lasti yea tu kwenye Confederesheni kapu...!

Nimeanza na mchano laivu kwa vile juzi kati nikiwa kijiweni, tulikuwa na ligi ndogo, kama kawa kama dawa niliwapa makavu waliobilivu eti Mayanki wa Anda Seventini wangeenda Kubrazuka kule kwa kina Neima...! Mi niliwachomoa mapema na kuwalia kiapo, HAWATIMBI hata kidogo! Unajua nini? Nilishasoma mchezo longtaim, mchongo wao wa kujazwa mzuka na wazee wa politiksi iliwatibulia.

Wabishi wakaniona mkuda na kunichana ooh..Mzee Baba we nuksi tu, huna uzalendo..., ila nikakazia kwa kubilivu, waiti itabaki waiti na blaki ni blaki tu...politiki kwenye ishu za maana ni msala!

Sasa buana hata wiki imekata basi, majanki si wale chaliii... Inauma, ila ishu ilianzia pale tu Wazee wa Politiksi waliposhadadia faino za Afkon anda seventini kwa vile tu eti zinapigwa Bongo. Fasta wakavaa kibwaya..ooh ndiki bee tu wana haoo wanakula mwewe na kwenda kubrazuka...! Wakafogeti tupo grupu moko na Wanaija, mayanki wa Mu7 na wale machalii wa kina Savimbi, tupenye? Mawee!

Ndiki zote walizopiga madogo walikuwa wakifili namna ya kudraivu mandinga yao...sijajua hadi tudei kulikuwa na sababu gani majanki kupewa ofa za namna hiyo wakati walipaswa kuandaliwa kisaikolojia ili wakinukishe kwanza, theni ndipo wapewe asante!

Tulijipa mahopu mengi, tukafogeti kufanya preparesheni ya maana hasa ikizingatiwa tulipenya faino hizi kama hosti, hatujapigika...!