Umesikia hii ya mabao ya Ubelgiji?

Sunday July 8 2018

 

STAA wa Ubelgiji, Dries Mertens amesema hivi watahakikisha wanafunga mabao zaidi yafika 16 kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018 ili wananchi wa huko kwao Ubelgiji warudishiwe pesa zao walizotumia kununulia televisheni kwa ajili ya kutazama michuano hiyo.

Ubelgiji kwa sasa imeshafunga mabao 14 na kutinga kwenye hatua ya nusu fainali, hivyo kama itafunga mabao mawili zaidi basi itakuwa sherehe kwa raia wa Ubelgiji ambao walinunua televisheni za kampuni ya Krefel katika kipindi hiki cha Kombe la Dunia kwamba watarudishiwa pesa zao.

Kampuni hiyo ya Krefel ilisema kwamba kama Ubelgiji itafunga mabao 16 kwenye Kombe la Dunia, basi walionunua televisheni zao kwenye kipindi hiki cha fainali hizo watarudishiwa pesa.

Advertisement