Terry kang’atuka, anataka kazi mpya

Tuesday October 9 2018

 

BEKI mbishi, John Terry ameamua kung’atuka kwenye soka kama mchezaji na sasa anajiandaa kwenda kuwa msaidizi wa Thierry Henry huko Aston Villa.

Wawili hao walikuwa maadui wakubwa kwenye Ligi Kuu England, wakati Chelsea ilipokuwa ikikumbana na Arsenal kwa sababu mmoja alikuwa beki wa kati na mwingine alikuwa mshambuliaji, kwa sasa hawatakuwa tena na upinzani watakuwa marafiki kuhakikisha Aston Villa inafanya kweli kama watafanikiwa kubamba dili la kuinoa timu hiyo. Henry anapewa nafasi kubwa ya kurithi mikoba ya Steve Bruce huko Villa Park.

Na Terry, ambaye hakuwa na timu tangu alipoachana na Aston Villa mwishoni mwa msimu uliopita, ameamua kustaafu uchezaji ili kwenda kuwa msaidizi wa Henry kwenye benchi la timu hiyo.

Terry, aliyewahi kuwa nahodha wa Chelsea na England alisema: “Baada ya miaka 23 ya kuwa mchezaji, nimeona ni wakati mwafaka wa kustaafu soka. Nasubiri tu kufungua ukurasa mpya wa maisha yangu na kukabiliana na changamoto mpya.”

Uamuzi huo wa Terry umezidi kuchochea uwezekano wa kwenda kuungana na Henry huko kwenye kiti cha ukocha wa Aston Villa.umpa mkataba mpya.

Advertisement