Simeone anamsajili Neymar sio Mbappe

Thursday September 13 2018

 

KOCHA wa Atletico Madrid, Diego Simeone amefichua akipewa nafasi ya kuchagua baina ya Neymar na Kylian Mbappe, chaguo lake hapo lipo wazi kabisa, atachukua huduma ya Mbrazili, Neymar.

Washambuliaji hao wote wanakipiga kwenye kikosi cha Paris Saint-Germain ndio wachezaji ghali zaidi kwa sasa kutokana na huduma zao kuwagharimu pesa nyingi sana mabingwa hao wa Ufaransa.

Neymar alitua PSG akitokea Barcelona na Mbappe alitua kwa wababe hao wa Paris akitokea AS Monaco, huku ushirikiano wao wa ndani ya uwanja ukileta matokeo mazuri kabisa uwanjani.

Neymar amefunga mabao 32 katika mechi 35 alizoichezea PSG, wakati Mbappe amefunga mabao 25 katika mechi 47 za michuano yote waliyokitumikia kikosi hicho cha mabingwa wa Ufaransa.

Mbappe ni mdogo kwa miaka saba kwa Neymar, lakini Simeone alisema: “Namchukua Neymar.

Kwenye ile Barcelona ya Luis Enrique, pale alipohitajika kufanya kazi, alifanya. Mbappe ni mbinafsi sana, pia ni mchezaji wa nafasi moja. Neymar anbabadilika, unamtumia kwenye nafasi nyingi.”

Advertisement