Ronaldo kumfikia Messi kwa tuzo

Tuesday December 5 2017

 

Paris. Ufaransa. Cristiano Ronaldo ‘atapokea tuzo ya tano ya  Ballon d’Or akiwa juu ya mnara wa Eiffel uliopo jijini Paris, Ufaransa Alhamisi hii’
Kwa mujibu wa picha zilizosambaa mtandaoni mwezi uliopita zilisema mpinzani wake kutoka Barcelona, Lionel Messi ndiye atakayetwaa tuzo hiyo.
Lakini taarifa kutoka Hispania sasa zimethibisha kuwa  Ronaldo atapokea tuzo hiyo Paris, kauli iliyoungwa mkono na rais wa Bernabeu, Florentino Perez.
Mreno huyo yupo katika msimu ambao hatousahau katika kikosi cha Real Madrid.
Siyo tu kwa mafanikio yake binafsi, lakini akiwa mafanikiwa kufunga mabao mawili katika mashuti 68 aliyopiga, mbaya zaidi Real kwa sasa ipo nyuma kwa point inane kwa vinara wa La Liga, Barcelona.
Ni msimu mbaya kwa vijana Zinedine Zidane katika ligi ya Hispania tangu 2008.
Hata hivyo, Ronaldo aliingoza klabu hiyo kuweka historia ya kutetea ubingwa wa Ligi ya Mabingwa.
Taarifa ya gazeti la Mundo Deportivo limedai David Ginola ndiye atakayemkabidhi Ronaldo tuzo hiyo na kulingana na Messi kwa kutwaa tuzo hiyo mara tano.