Ukame wa mabao waandama Benzema, Ronaldo

Muktasari:

Jumamosi iliyopita  walipoteza nafasi nzuri ya kuwafanya kurudi katika mstari wa mbio za ubingwa hasa baaada ya Barcelona kupoteza pointi dhidi ya Celta Vigo.

Madrid, Hispania. Cristiano Ronaldo na Karim Benzema wamecheza jumla ya mechi 20 za LaLiga, ikiwa ni jumla baada ya kila moja kucheza mechi kumi, lakini wamefanikiwa kufunga mabao manne ikiwa ni takwimu yao mbaya zaidi ndani ya Real Madrid.
Jumamosi iliyopita  walipoteza nafasi nzuri ya kuwafanya kurudi katika mstari wa mbio za ubingwa hasa baaada ya Barcelona kupoteza pointi dhidi ya Celta Vigo.
Real Madrid kushindwa kutumia nafasi nzuri waliyopewa na miamba ya Catalonia na kushindwa kufunga dhidi ya Athletic Club ambayo ilitolewa katika Kombe la Mfalme katikati ya wiki na timu ya daraja la tatu Formentera. Kumeifanya Real kubaki nyuma kwa point inane kwa vinara Barca.
Matatizo ya ufungaji yapo wazi. Huku mwanachama wa tatu wa  BBC, Gareth Bale, akiwa na majeruhi yasiyokwisha, pamoja na kupoteza umakini katika umaliziaji.
Ronaldo ameondoka katika kufunga bao katika kila mashuti 4.6 msimu  2014/15 (yaliyofanya kuweka rekodi ya kufunga mabao 48 kwa msimu) sasa anahitaji kupiga mashuti 34 kushangilia bao moja msimu huu.
 Hizo ni takwimu mbaya kwake ikimrudisha katika msimu wa wa 2009/10, wakati alipokuwa akifunga bao moja kila baada ya kupiga mashuti 8.1.
Kwa upande wa Benzema hali yake ni mbaya. Amepiga mashuti 21 kufunga mabao mawili ukiwa ni wastani wa mashuti 10.5 kwa bao moja, Wakati katika msimu wa 2014/15 aliitaji mashuti manne kufunga bao moja iliyomfanya kumaliza msimu akiwa amefunga mabao 24.