Real Madrid vs Totteham zatangulia 16 bora Ligi ya Mabingwa

Tuesday December 5 2017

 

Hispania. Real Madrid itaikaribisha Borussia Dortmund kwenye mchezo wa mwisho katika makundi lakini ikiwa tayari imejihakikishia kucheza hatua ya 16 ya makundi.
Nayo Tottenham itaikaribisha APOEL Nicosia kwenye mchezo utakaopigwa kesho hiyo hiyo Jumatano.
Dortmund na APOEL zitashuka uwanjani kukamilisha ratiba hiyo huku tayari zimepoteza nafasi ya kufuzu kucheza 16 bora Ligi ya Mabingwa.