Mustafi ashangalia ushindi wa Arsenal mtupu!

Muktasari:

  • Arsenal imejiimarisha nafasi ya tatu baada ya kucheza michezo 9 huku ikiwa imeshakusanya pointi 21 sawa na Tottenham na Chelsea lakini zikitofautiana nafasi kutokana na mabao ya kufunga na kufungwa.
  • Man City ndiyo imejiweka kileleni ikiwa na alama 23 huku ikifuatiwa na Liverpool yenye alama 23

ENGLAND. Nyota wa Arsenal, Shkodaran Mustafi amejikuta akishindwa kujizuia furaha yake baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa jana Jumatatu usiku.
Mustafi alionekana kwenye video akicheza akiwa amevua bukta yake katika chumba cha kubadili nguo. Nyota huyo alikuwa amebakiwa na nguo ya ndani pekee, huku akipewa sapoti na wachezaji wanzake.
Alex Iwobi ambaye aliibuka kinara kwenye mchezo huo, naye alionekana akicheza na akiwa ameshika zawadi yake aliyokabidhiwa jana.
Ushindi huo wa Arsenal umepokewa vyema na mashabiki wao kutokana na kujihakikishia michezo yake iliyocheza hivi karibuni kutopoteza. Nyota wa mchezo huo wa jana, Alex Iwobi alimtunuku baba yake zawadi aliyoipokea kutokana na kuibuka kinara kwenye mchezo huo wa jana Jumatatu.
Ushindi huo wa jana umeendeleza kasi ya kocha Unai Emery ya kutopoteza michezo ambayo kikosi chake kimeshuka dimbani hivi karibuni.
Mabao ya Arsenal yalifungwa na Mesut Ozil (45’), Pierre –Emerick Aubeyang (63’ na 66’)