Mourinho amtwisha zigo Martia kuimaliza Juventus

Muktasari:

  • Martial anatajwa kutokuwa na muda mrefu kuendelea kuitumikia Man United, ambapo inaelezwa kuwa ni miongoni mwa wachezaji wanaosemekana huenda wakafungasha virago msimu ujao  wa kiangazi.

 

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ametamka wazi kwamba mchezaji wake Anthony Martial ajiandae kwenye kikosi cha kwanza kitakachoanza katika mchezo dhidi ya Juventus leo Jumanne usiku.

Miamba hiyo ya soka ya Italia itakuwa na kibarua kigumu ambapo Man United iakuwa ikijaribu kulinda heshima kwenye uwanja wake wa nyumbani, Old Trafford.

Tayari Jose Mourinho ameanza kutangaza silaha zake za kuimaliza Juventus baada ya kumweleza Martial kuwa ataanza kwenye kikosi cha leo usiku dhidi ya Juventus.

Nyota huyo anashuka dimbani kuikabili Juventus huku akiwa na rekodi nzuri ya mchezo uliopita ambapo aliiwezesha timu yake kupata mabao mawili ambayo yote aliyatupia wavuni, walipokutana na Chelsea Jumamosi wiki iliyopita.

Hata hivyo mabao hayo yakarudishwa na wapinzani wao huku Ross Barkley akiisawazishia timu yake bao la usiku na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya mabao 2-2