Morata, Rashford usipime kabisa

Tuesday November 20 2018

 

London, England.WAKAA benchi, Manchester United, Marcus Rashford na mwenzake Alvaro Morata wa Chelsea wameonyesha kukaa kwao benchi au kuanzia benchi kufike mwisho baada ya kupandisha thamani zao mwishoni mwa wiki kwa kuzibeba timu zao za taifa.

Rashford hayuko sana kwenye mipango ya kocha wa timu yake, Jose Mourinho na amekuwa akianzia benchi au kukosa namba kabisa.

Hata hivyo, nyota huyo, juzi alimwonyesha mchezaji Bora wa Kombe la Dunia, Luka Modric kuwa yeye ni kati ya wachezaji tishio alipoiongoza England kuilaza Croatia mabao 2-1 mechi ya Ligi ya Uefa kwa Mataifa ya Ulaya kwenye Uwanja wa Wembley.

Straika huyo wa Manchester United alionekana mwenye kasi akipandisha mashambulizi ya mfululizo hasa dakika 45 za kwanza huku akishangiliwa kwa nguvu na mashabiki wake.

Katika mchezo huo ambao England ilitoka nyuma, Modric licha ya kucheza mpira mwingi ambao kila mmoja aliamini atamfunika Rashford, lakini mchezaji huyo alionyesha soka ya kiwango na kumficha kabisa Modric. Kiwango chake pia kilishangiliwa na mashabiki wa timu Manchester United mara zote.

Naye Alvaro Morata wa Chelsea aliifungia Hispania bao murua ilipopata ushindi wa bao 1-0 mechi ya kirafiki dhidi ya Bosnia and Herzegovina juzi.

Morata, 26, anayechezea Chelsea ambaye amefunga mara tatu katika mechi tatu, alisema kufunga kwake kumemsaidia kumtengenezea mazingira ya kujiamini kwani timu yao ilifungwa mabao 3-2 na Croatia na alifunga bao dhidi ya Bosnia and Herzegovina.

Chini ya saa moja, Hispania ilikuwa ikishambulia mbele ikiongozwa na Marco Asensio ambaye alitoa pasi iliyomfikia Morata na kufunga bao hilo.

Ilikuwa rahisi kwa Morata kufunga kutokana na mabeki wa Bosnia kujichanganya wenyewe katika harakati za kujaribu kuokoa.

Advertisement