Mastaa Chelsea wamsubiri kocha mpya

Saturday June 22 2019

 

By THOMAS NG'ITU

BAADA ya kocha Maurizio Sarri kuachana na Chelsea, wachezaji wa klabu hiyo wanamsikilizia bosi wao  Roman Abramovich kuwaletea kocha mwingine msimu ujao.
Baada ya kocha huyo kuondoka mara kwa mara nyota wa zamani wa klabu hiyo, Frank Lampard amekuwa akitajwa kurithi mikoba licha ya kwamba haijawa rasmi.
Inatajwa kwamba mabosi wa Chelsea tayari wameanza kuzungumza na Lampard kurithi mikoba ya Sarri aliyetimkia klabu ya Juventus.
Wakati timu hiyo ikiwa bado haijapata kocha, inatarajiwa kuanza maandalizi ya msimu mpya kwa kucheza mchezo wa kirafiki Julai 10, Florida nchini Marekani
Mpaka hivi sasa hesabu zote zipo kwa kiungo wao wa  zamani, Lampard lakini mabosi wa klabu yake ya Derby County nao hawajakubali kumuachia mpaka sasa kutokana na jinsi ambavyo anaishi na wachezaji wa timu hiyo.

Advertisement