Advertisement

Manchester City, United zamwania Ruben Neves

MANCHESTER United na Manchester City zimeingia katika vita ya kumwania kiungo mahiri wa Wolves na Timu ya Taifa ya Ureno, Ruben Neves na zote zitaweka noti mezani katika dirisha la Januari kwa ajili ya kujaribu kumtwaa.

IN SUMMARY

Machester City inaongeza kasi zaidi baada ya kumkosa Jorginho aliyekimbilia Chelsea akitokea Napoli katika dirisha kubwa lililopita la majira ya joto huku Kocha, Pep Guardiola akiwa na wasiwasi na umri wa kiungo, Fernandinho ambaye ana umri wa miaka 33.

Kwa upande wa Manchester United, Kocha Jose Mourinho anamtaka staa huyo Mreno kwa ajili ya kukiongezea makali kikosi chake ambacho bado kinayumba katika Ligi Kuu England licha ya kumnasa kiungo wa Brazil, Fred kutoka Shakhtar katika dirisha kubwa lililopita.

More From Mwanaspoti
Advertisement
This page might use cookies if your analytics vendor requires them. Accept