Man United yaweka ubaoni mabeki nane

Muktasari:

Tangu mwaka huu ulipoingia, kocha Jose Mourinho amekuwa na mpango wa kukiboresha kikosi chake ili kuwa na uwezo wa kushindania mataji msimu ujao.

MANCHESTER United imeripotiwa kuweka majina nane ya mabeki wa kati kwenye orodha yao ya wale inaotaka kuwasajili kabla ya msimu mpya wa Ligi Kuu England kuanza mwezi ujao.

Tangu mwaka huu ulipoingia, kocha Jose Mourinho amekuwa na mpango wa kukiboresha kikosi chake ili kuwa na uwezo wa kushindania mataji msimu ujao.

Kwa mujibu wa ripoti zilizopatikana ni kwamba Man United inawafanyia tathmini mabeki wa kati mwenye umri kati ya miaka 23 na 29 ili kupata wanaofaa wa kuwanasa kuja kuifanya timu yao kuwa tishio kwenye michuano ya England na Ulaya. Mabeki hao wanaosakwa na Mourinho ni Raphael Varane, Jose Gimenez, Alessio Romagnoli na Milan Skriniar, ambao itabidi afanye kazi kweli kweli kuwapata kwa sababu kuna dalili zote za mabeki hao wakabaki kwenye timu zao.

Mabeki wengine ni Toby Alderweireld, Kalidou Koulibaly, Jerome Boateng na Caglar Soyuncu, ambao Mourinho anaamini akiwapata atakuwa amefunga rasmi duka lake kwenye kusajili mabeki.