Maguire achekelea kutua Man United

Monday August 5 2019

 

MANCHESTER, ENGLAND. Harry Maguire ni mchezaji rasmi wa Manchester United. Mchezaji huyo amesaini mkataba wa miaka sita kwa ada ya Pauni 80 milioni.
 Usajili huo unamfanya nyota huyo kuwa beki wa thamani zaidi duniani na atakuwa akilipwa mshahara wa Pauni 200,000 kwa wiki.
 Baada ya kunaswa Maguire aliuamimbia mtandao wa klabu ya Manchester United; “Nimefurahi kusajiliwa katika klabu kubwa. Nilikuwa na wakati mzuri nikiwa na Leicester City na ninamshukuru kila mtu kwa jambo hilo.
 “Pamoja na yote, klabu kama Manchester United inapokuja mlangoni kwako kukupigia hodi, huo ni wakati mzuri.
“Nimezungumza na kocha, ameniambia mitazmo ya klabu hii ya mbele. Nimefurahi kukutana na mipango mizuri. Ni wazi kwamba kocha (Ole) yupo katika mipango kabambe ya kutengeneza kikosi.
 Nina shauku ya kukutana na wachezaji wenzangu na kuanza msimu.
Naye kocha Ole Solskjaer aliongeza: “Harry ni mmoja kati ya mabeki wa kati hodari. Nimefurahi kuona kwamba tumepata saini yake.”

Advertisement