Liverpool yageuzia rada kwa kipa Alisson

Wednesday July 18 2018

 

Klabu ya Liverpool inakaribia kumsajili kipa wa Roma, Alisson kwa dau la Pauni 62 milioni kwenye dirisha hili la msimu wa kiangazi.
Kocha Jurgen Klopp tayari ameonyesha nia ya kuhitaji huduma ya mlinda mlango huyo ili kumuweka kuwa kipa namba moja kikosini hapo kutokana na Loris Karius kushindwa kumshawishi.
Alisson mwenye miaka 25 amekuwa kwenye kiwango kizuri tangu msimu uliopita, huku akihakikishiwa mkataba kwenye klabu yake ya Roma.
Kipa huyo raia wa Brazil yupo nchini mwake akiwa mapumzikoni pamoja na familia yake.

Advertisement